Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwanza kabisa michezo ni njia ya pekee ya kuufanya ubongo kuchangamka na kufanya kazi vizuri, kama mwanadamu ukijitahidi angalau ukatengane muda mchache wa mazoezi utakuwa ni mwenye afya na nguvu katika maisha yako
 
Unakuwa na afya : ukiwa kama mwana michezo ndani ya jamii kwanza unakuwa na afya ya kutosha katika mwili wako, na wafanya mazoezi wengi ukiwaangalia tuu macho lazima utafikiria kwamba uyu ni mwana mazoezi bila kipingamizi chochote kile, kwasababu mili yao inakuwa naukakamavu wa kutosha na afya tele.
 
Ni vigumu kupata maradhi mara kwa mara : pili kama wew ni mwana mazoezi au michezo utakubaliana nami katika hili kwamba mtu yeyote anae fanya mazoezi ni vigumu sana kupata maradhi ya mara kwa mara kwasababu ya mazoezi anayofanya.
 
Mwenye furaha muda wote : pia ukiwa mwana maozezi muda wote unakuwa nafuraha tu, ni wachache sana huwa hawana furaha lakini asilimia kubwa ya wanamichezo akili inakuwa inatulia hivyo kwao michezo ni furaha pia.
 
Michezo ni ajira : pia faida nyingine ya kuwa mwana michezo inaajiri watu, baadhi ya wana michezo duniani wamefanya michezo hiyo kama ajira kwao na inawalipa vizuri mfano mzuri ni mchezaji wetu wa mpira wa miguu mmbwana samatta kwake michezo ni ajira nzuri na inamlipa vizuri sana, hivyo basi kama wew una kipaji na mchezo wowote kifufue na ipo siku utafurahia kuwa mwana michezo ulimwenguni kote.
 
Faida za michezo kwa vijanaHapa kuna orodha ya faida ambazo vijana hupata kutoka kwa michezo:Shughuli ya kawaida ya kimwiliMichezo inaruhusu vijana kushiriki katika shughuli nyingi za mwili kama vile kukimbia, kuruka, kupiga mbizi, kutupa na zaidi.
 
Inaboresha ujuzi wa kutatua matatizo

Kila mchezo wa mashindano kwa njia isiyo ya moja kwa moja hufundisha jinsi ya kushinda changamoto. Vijana ambao hucheza michezo hukaribia kila changamoto na hali ya akili kutafuta njia za kushinda changamoto hiyo.
 
Weka msingi thabiti wa maisha yenye afya

Mazoezi ya kawaida ni moja ya funguo za maisha marefu na bora. Mchezo husaidia vijana kupunguza hatari ya kuathirika na magonjwa fulani wakati wa uzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…