Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Chukulia kwamba mtu unayemsikiliza kuna kitu anachojua ambacho wewe hujui.Ukweli ni kwamba kila mtu kuna kitu anajua ambacho wewe hujui, hivyo unapofanya mazungumzo na yeyote, sikiliza kwa makini sana. Mtu yeyote atakuambia chochote unachotaka kujua, kama utasikiliza kwa makini.
 
Kuwa makini na watu unaowashirikisha habari zako nzuri.Wengi unaofikiri wanakupenda na kukujali, wanaweza kugeuka watu wabaya sana pale wanaposikia habari zako nzuri.
 
Chukulia kwamba mtu unayemsikiliza kuna kitu anachojua ambacho wewe hujui.Ukweli ni kwamba kila mtu kuna kitu anajua ambacho wewe hujui, hivyo unapofanya mazungumzo na yeyote, sikiliza kwa makini sana. Mtu yeyote atakuambia chochote unachotaka kujua, kama utasikiliza kwa makini.
 
Weka juhudi kuimarisha mahaba kwenye mahusiano yako.Mahusiano ni kazi na kila kazi inahitaji juhudi. Kuweza kuwa na mahusiano bora na mwezi wako, unahitaji kuweka juhudi katika kujenga mahusiano hayo.
 
Kuwa makini na unaowashirikisha habari zako mbaya.Wapo watakaoonekana kusikitika lakini moyoni wanafurahia unapokuwa kwenye matatizo, kuwa makini na unaowashirikisha habari zako mbaya.
 
Fanya angalau kitu kimoja kuwa bora kila mahali unapoenda.Usiende sehemu yoyote halafu ukaondoka hujabadili kitu chochote kikawa bora, itakuwa haina maana yoyote ya wewe kuwepo eneo hilo. Angalia kipi unaweza kuboresha zaidi popote ulipo, kisha boresha.
 
Tengeneza taswira ya unataka kuwa nani, kisha weka juhudi kufikia taswira hiyo.Watu wengi hawajui nini wanataka kwenye maisha yao hivyo wanajiendea tu. Usiwe wewe, jua unataka kuwa nani, unataka kufikia wapi, kisha kila siku weka juhudi kufika pale unapotaka kufika.
 
Usijiruhusu kuwa na kiburi au hasira.Hizi ni hisia mbili ambazo zitakuharibia sifa yako, kuvuruga mahusiano yako na wengine na kukuingiza kwenye matatizo makubwa, usikubali hisia hizo zikutawale.
 
Jaribu kufanya chumba kimoja kwenye nyuma yako kuwa kizuri iwezekanavyo.Kwenye nyumba unayoishi, kazana kufanya chumba kimoja kuwa kizuri sana kiasi kwamba kila wakati utapenda kuwa kwenye chumba hicho, kisha kifanye kuwa eneo lako la kupumzika au kutafakari maisha yako.
 
Jilinganishe na ulivyokuwa jana, na siyo kujilinganisha na wengine walivyo leo.Kosa kubwa unaloweza kufanya kwenye maisha yako, ni kujilinganisha na mtu mwingine yeyote, awe yupo juu yako, chini yako au sawa na wewe. Mtu pekee wa kujilinganisha naye ni wewe mwenyewe, kama leo umefanya kwa ubora kuliko jana unapiga hatua, kama umefanya kama jana unarudi nyuma, kama umefanya chini ya ulivyofanya jana hujui unachofanya.
 
Weka juhudi kubwa uwezavyo kwenye angalau eneo moja kisha angalia nini kitatokea.Kwenye maisha yako, chagua eneo moja ambalo utaweka juhudi kubwa sana, utakwenda hatua ya ziada, utafanya kila kinachopaswa kufanyika, kisha angalia matokeo utakayopata, yatakuwa matokeo bora, makubwa na ambayo yatakupa hamasa ya kuendelea na juhudi zaidi kwenye maeneo mengine ya maisha yako.
 
Kama kumbukumbu za nyuma zinakufanya ulie, ziandike kwenye karatasi kwa umakini na ukamilifu.Kumbukumbu tunazobeba, zinaweza kuwa mzigo mzito kwetu na unaoturudisha nyuma, tunahitaji kuutua. Kitendo cha kuandika kitu, unakuwa umekitua kutoka kwenye akili yako na kinaacha kuwa mzigo.
 
Imarisha muungano wako na watu.Unahitaji kuwa na mtandao wa watu ambao wanaweza kukusaidia kwenye maeneo mbalimbali na wewe pia unaweza kuwasaidia. Imarisha muungano na mahusiano yako na wengine.
 
Usikebehi taasisi za kijamii.Hata kama hukubaliani na mtu au watu, usiwakebehi, kuwadharau au kuwakosoa kwa namna ya kudhalilisha. Hii inakwenda kuanzia kwenye taasisi mbalimbali kama za kidini na hata kwa watu binafsi.
 
Jichukulie kama mtu ambaye una jukumu la kumsaidia.Tunapopewa kazi ya kuwasaidia wengine, tunafanya kazi nzuri sana, lakini kwetu sisi wenyewe hatufanyi kazi nzuri. Jichukulie wewe kama mtu uliyepewa jukumu la kumsaidia kisha msaidie hasa.
 
Waombe watu wakusaidie kitu kidogo ili nao wakuombe uwasaidie kitu.

Maisha ni mahusiano, kadiri mahusiano yako na wengine yanavyouwa bora, ndivyo maisha yako yanavyokuwa bora. Na mahusiano yanaimarishwa kwa namna watu mnashirikiana na kusaidiana, waombe watu wakusaidie kitu, ili nao wawe tayari kukuomba uwasaidie kitu.
 
Tengeneza urafiki na watu wanaotaka ufanikiwe.

Wale wanaokuzunguka wanaweza kuwa kikwazo kikubwa sana kwa mafanikio yako. Kama umezungukwa na watu waliokata tamaa, na wewe utakata tamaa.
 
Usijaribu kumwokoa mtu ambaye hataki kuokolewa, na kuwa makini unapomwokoa mtu ambaye anataka kuokolewa.

Kuna sababu kwa nini mtu ameingia kwenye matatizo ambayo unamwona anapitia. Ukikazana kumwokoa mtu ambaye yupo kwenye matatizo, bila ya kujua sababu iliyomwingiza kwenye matatizo hayo, unajiingiza mwenyewe kwenye matatizo.
 
Hakuna kitu kilichofanywa vizuri ambacho hakina maana.

Kitu chochote ambacho kimefanywa vizuri, hata kama ni kidogo kiasi gani, kina maana kubwa sana. Fanya kila kitu vizuri, hata kama ni kidogo.
 
Iweke nyumba yako vizuri kabla hujakosoa dunia.

Kukosoa ni rahisi, lakini kuchukua hatua ni kugumu. Tunaishi kwenye dunia ambayo kila mtu anaweza kukosoa wengine, lakini yeye mwenyewe maisha yake yanamshinda. Nyoosha kwanza maisha yako kabla hujajipa jukumu la kuinyoosha dunia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…