ISIS
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 96,072
- 858,588
Sawasawa!Ni vigumu kuelezea moja kwa moja kujiamini maana yake nini? Lakini mtazamo wa mwanadamu juu ya namna wenzake wanavyomchukulia inaweza kuwa kutafsiri ya neno kujiamini
👍Kujizoeza kujiamini
Njia moja muhimu sana kisaikolojia ya kujenga hali ya kujiamini ni kupenda kusikiliza maneno ya kutia moyo nay a ujasiri kutoka kwa watu maarufu. Kwa mfano, viongozi wenye msimamo, watetezi wa haki za binadamu, wanasiasa wanaotetea maslahi ya nchi bila hofu na kadhalika. Hotuba na maneno yao yakipata sehemu kubwa katika akili ya mtu, lazima yatajenga hali ya kujiamini kama wale anaowasikiliza.
Nakazia ✍️✍️✍️Yafuatayo ni mambo 40 muhimu kuzingatia kwenye maisha
Sema ukweli.
Nafikiri hili halina haja ya maelezo marefu, sema ukweli mara zote, usidanganye hata kama ni kitu kidogo kiasi gani, sema kweli na kweli itakuweka huru. Ukweli ni rahisi kukumbuka na ukweli utakuweka sehemu salama mara zote.
KweliKuwa makini na watu unaowashirikisha habari zako nzuri.Wengi unaofikiri wanakupenda na kukujali, wanaweza kugeuka watu wabaya sana pale wanaposikia habari zako nzuri.
Aisee!Usijaribu kumwokoa mtu ambaye hataki kuokolewa, na kuwa makini unapomwokoa mtu ambaye anataka kuokolewa.
Kuna sababu kwa nini mtu ameingia kwenye matatizo ambayo unamwona anapitia. Ukikazana kumwokoa mtu ambaye yupo kwenye matatizo, bila ya kujua sababu iliyomwingiza kwenye matatizo hayo, unajiingiza mwenyewe kwenye matatizo.
AmenMungu atupe afya na uzima 🙏 🤲