Kuamini kila kinachosemwa na “Wataalamu”
Siku hizi kila sekta kuna watu wanaojiita wataalamu (mimi mmoja wapo!) Lakini nasikitika kukuambia kuwa, wengi wa wataalamu hawa, hawako sahihi kwani siku hizi watu wanapata kipato kutokana na kuyaelewa matatizo ya watu na si kujua suluhisho.
Usimuamini mtu eti tu kwa kuwa analielezea kwa uzuri na analielewa tatizo lako bali muamini anayeweza kutoa suluhisho linalokuwa msaada kwa tatizo lako
Usimuamini mtu eti tu kwa kuwa analielezea kwa uzuri na analielewa tatizo lako bali muamini anayeweza kutoa suluhisho linalokuwa msaada kwa tatizo lako
Kuhisi huwezi kwa kuwa kuna mtu anakuambia hivyo
Kuna watu maishani wapo sii tu kwa kukukwamisha wewe, bali pia kumkwamisha kila anayewazunguka. Ukiona hakubaliki kwa jinsi ulivyo, basi jua huko mahali sahihi. Usikubali kuishi kama mtu mwingine kwa kuwa tu unataka kukubalika maishani.
Kuona huhitaji chochote cha kusoma
Maisha yanachekesha! Kitu kinaweza kuwepo leo, na kesho kisikuwepo. Kama kuna kitu unataka kufanya, fanya sasahivi. Kama ni wazo la muda mrefu, basi anza leo kutekeleza kidogo kidogo. Kila muda una changamoto zake. Hata tajiri mkubwa duniani Bill gates anachangamoto zake kulingana na nafasi aliyonayo