Jiandae kisaikolojia
Kustaafu ni kipindi tofauti sana na kipindi ulichokuwa kwenye ajira. Kipindi hiki utakutana na mtindo mpya wamaisha tofauti na ule uliouzoea.
Ni muhimu kujiandaa kisaikolojia kwa maswala kama vile kukaa bila kupata mshahara, ofisi, gari la kampuni au taasisi, nyumba ya taasisi au kampuni pamoja na manufaa mengine ya wafanyakazi
Weka akiba
Ikiwa kazi yako ndiyo uliyokuwa unaitegemea kama chanzo chako cha kipato, basi tafakari juu ya maisha bila kazi hiyo. Hakikisha unaweka akiba ya kutosha itakayokuwezesha kumudu matumizi yako mbalimbali baada ya kustaafu.
Lipa madeni
Kumbuka baada ya kustaafu kiwango chako cha kipato kitapungua; hivyo ni muhimu kulipa madeni kabla ya kustaafu ili usije ukahangaishwa na madeni wakati wa kustaafu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.