Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Chelsea wameanza mazungumzo na Sevilla kuhusu kumsajili beki wa Ufaransa mwenye thamani ya pauni milioni 50 Jules Kounde, 23, ambaye aliisaidia klabu hiyo ya Uhispania kushinda Ligi ya Europa mwaka 2020. (Sport - in Spanish)
 
Wolves wanakaribia kumsajili Joao Palhinha wa Sporting Lisbon, huku kiungo huyo wa kati wa Ureno, 26, akikubali kujiunga kwa mkataba wa muda mrefu kwa ada ya takriban £20m. (Sun)
 
Manchester City wanasalia kumtaka kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 26, lakini Leeds United bado wana matumaini ya kumbakisha mchezaji huyo baada ya kuepuka kushushwa daraja. (Sun)
 
Real Madrid wanamtaka kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Uingereza Jude Bellingham, lakini hawatamnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 hadi 2023. (Bild - in German)
 
Manchester United wamemtanguliza mlinzi wa Ajax na Uholanzi Jurrien Timber, 20, lakini pia wamefanya duru mbili za mazungumzo na mlinzi wa Braga Mreno David Carmo, 22. (Manchester Evening News)
 
Villarreal wapo kwenye mazungumzo ya juu ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Giovani lo Celso kwa mkataba wa kudumu kutoka Tottenham. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na klabu hiyo ya Uhispania kwa mkopo mwezi Januari. (Football Insider)
 
Aston Villa wanataka wachezaji wengine watatu baada ya kumuongeza kiungo wa kati Mfaransa Boubacar Kamara, 22, kutoka Marseille, beki wa kati wa Brazil Diego Carlos, 29, kutoka Sevilla na kubadilisha uhamisho wa mkopo wa fowadi wa Brazil Philippe Coutinho, 29, kutoka Barcelona kuwa usajili wa kudumu.
 
Mshambulizi wa Uruguay mwenye umri wa miaka 35, Luis Suarez, ambaye anaondoka Atletico Madrid, ni mmoja wa wale wanaozingatiwa. (The Athletic - subscription required)
 
Back
Top Bottom