Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Barcelona wamemwambia mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, 29, kwamba anaweza kujiunga nao kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake na Reds utakapomalizika msimu ujao. (Mirror)
 
Tottenham wanajiandaa kuongeza juhudi za kumsaka beki wa Middlesbrough Muingereza Djed Spence, 21, ambaye alikuwa Nottingham Forest kwa mkopo wa msimu mzima. (Express)
 
Liverpool wamemaliza nia yao ya kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona mwenye umri wa miaka 17 raia wa Uhispania Gavi. (Sport - kwa Kihispania)
 
Kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic, 33, atajiungfa na Roma kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wake utakapomalizika Manchester United mwisho wa mwezi huu wa Juni. (Sky Sports)
 
Chelsea huenda ikasaidia kumshawishi mchezaji wao Declan Rice, 23, kurejea nyumbani kutoka klabu ya West Ham kwa kumpatia kiungo huyo wa kati wa Uingereza fulana nambari 41 mgongoni. (Express)
 
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Mateu Alemany anatazamiwa kuruka kuelekea Uingereza wiki hii kuanza mazungumzo na Leeds kuhusu mpango wa kumnunua fowadi wa Brazil Raphinha, 25. (Sport, via Mail).
 
Newcastle wamemfanya mlinzi wa Atletico Madrid raia wa Brazil Renan Lodi, 24, kuwa chaguo lao la kwanza kuziba pengo la beki wa kushoto. (Jacque Talbot, kupitia Give Me Sport)
 
Chelsea wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsaka mshambuliaji wa Barcelona na Ufaransa Ousmane Dembele, ambaye atapatikana bure baada ya mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 utakapokamilika mwezi Juni. (Talksports)
 
Manchester United wanatumai kwamba wanaweza kumnasa mchezaji wa Denmark Christian Eriksen kwa uhamisho huru kufuatia mkataba wake wa muda mfupi na Brentford kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni. (Mirror)
 
Arsenal wako tayari kumpa mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus, 25, mshahara wa wiki wa pauni 190,000 ili kuhamia Emirates Stadium msimu huu wa joto. (Sun)
 
Liverpool wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumnunua winga wa Leeds na Brazil Raphinha, 25, baada ya tetezi za kuondoka msimu huu kwa mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, 30, kuzidi kuongezeka. (Sun)
 
Mane amesisitiza kuwa anataka kuondoka, huku mshambuliaji huyo akihusishwa na Bayern Munich, akikaa kimya bila kudai chochote kuhusu kandarasi kwenye uongozi wa juu wa Anfield. (Daily Telegraph)
 
Meneja wa Roma Jose Mourinho, 59, ameibuka kuwa mpinzani wa Zinedine Zidane kuwania nafasi ya Mauricio Pochettino kama meneja wa Paris St-Germain. (Daily Mail)
 
Back
Top Bottom