Kuna msemo unaosema cheka uongeze siku za kuishi, msemo huu umekua proved na wataalamu wengi wa afya na saikolojia ya mwanadamu kuwa uana ukweli ndani yake.
mara nyingi mtu anapotabasamu ama kufurahi kuna homoni anazi stimulate ambazo zinamsaidia katika maisha yake na mazingira yanayo mzunguka na kufanya maisha kuwa rahisi.
Jivunie jinsi ulivyo pamoja na kuwa wewe, kwani katika watu zaidi ya bilioni 7 ulimwenguni hakuna hata mmoja ambae yuko kama wewe. Hivyo unapaswa kufarahi kuwa wewe pamoja na sifa zote ulizo nazo.
Vuta picha nzuri juu ya maisha yako pamoja na vitu vyote vinavyokuzunguka, walimwengu wanasema hakuna kibaya bali ni macho na mtazamo wa mtazamaji. Kweli kabisa naungana nao kwani wewe ni mzuri na usikubali mtu akwambie vinginevyo.
Unapotaka kutambua nini maana ya kua na furaha muda wote maishani mwako inakubidi kwanza uwe mvumilivu na mwenye subira, kwani kila kitu hutokea kwa wakati wake.
Tengeneza familia yenye furaha (Happily Family).
Kwanza kabisa kama mtu ambae ungependa kuwa na furaha maishani basi anza na kutengeneza furaha ndani ya familia yako ambao ni watu wako wa karibu kabisa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.