Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuamini watoto wetu hawana makosa (wamekamilika)
Tatizo kubwa ninalolisikia kutoka kwa walimu, washauri, wasichana wa kazi, au walezi wengine wa watoto kwenye mashule na majumban ni kwamba wazazi wengi hawapendi kusikia mambo hasi (ubaya) yanayohusu watoto wao. Wengi hudai watoto wao hawako hivyo, wakisahau kuwa wao wametingwa na majukumu mbalimbali na hawajui maendeleo yoyote ya mtoto!
Wa kwanza kulaumiwa huwa ni mlezi huyo na mzazi hukaa upande wa mtoto. Matokeo yake mtoto hatamsikiliza mlezi wake tena kwani anajua mzazi yuko upande wake!
 
Kutowapa nafasi ya kucheza Utotoni
Ulishawahi kurudi nyumbani ukakuta kuta zako zote za nyumba zimechorwa vipepeo, midoli na kubandikwa stika mbalimbali ? Je, ulichukua hatua gani? Ukweli ni kwamba hiyo ni moja ya Baraka uliyopewa kushirikiana maisha na viumbe hawa wadogo. Siku moja hakutakuwa na michoro ukutani, wala midoli kitandani kwako, hutasikia kelele za aina yoyote na utajiona mpweke watakapokwenda kuanzisha familia zao.
Tunahitaji kuwapa watoto muda mwingi wa kucheza na wenzao kwani hii huwapa nafasi ya kuzijua kalama na vipaji vyao. Pia huwapa watoto hali ya kujiamini na kufanya maamuzi.
 
Wazazi Kutokua Kitu Kimoja
Kama nilivyosema hapo juu, hakuna mwalimu wa muhimu kama mzazi, na mtoto anahitaji malezi ya pande zote pili ikizingatiwa nae atakuwa mzazi siku moja. Wengi wa wazazi huangalia zaidi namna ya kuwatimizia mahitaji watoto nakusahau maisha yao binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…