Parachichi lina Fatty Acid
Fatty Acid ni asidi itokanayo na mafuta ya parachichi ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya shughuli mbalimbali katika miili yetu.
Hupunguza lehemu mbaya (cholesterol)
Mafuta ya lehemu ni hatari ikiwa kiwango chake kitakuwa kingi mwilini; mafuta haya husababisha matatizo mbalimbali hasa maradhi ya moyo.
Hulinda afya ya moyo
Madini ya potasiamu yanayopatikana kwenye tunda la parachichi kwa zaidi ya asilimia 14 ni muhimu sana katika utendaji kazi wa misuli ya moyo.
Parachichi lina Potasiamu nyingi kuliko ndizi
Watu wengi wanapenda ndizi kwa kuwa ni chanzo kimoja wapo cha madini ya potasiamu, lakini hawafahamu kuwa ndizi ina potasiamu asilimia 10 na parachichi lina asilimia 14. Hivyo parachichi ni bora zaidi.
Potasiamu ni muhimu katika miili yetu kwani hutuwezesha kutawala kiwango cha sodiamu katika miili yetu na kutuepusha na madhara yatokanayo na madini haya ya sodiamu.
Huboresha afya ya nywele na ngozi
Naamini umewahi kusikia kuwa parachichi hutumika kutengenezea mafuta ya nywele na ya ngozi; hii ni kutokana na kusheheni vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya nywele na ngozi zetu
Huzuia saratani
Tafiti zilizofanyika zimebainisha kuwa kula matunda ya parachichi kunasaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa seli za saratani ya tezi dume.
Huimarisha mifupa
Kutokana na parachichi kuwa na vitamini K pamoja na madini ya kopa na folate ambavyo ni muhimu kwa ajili ya mifupa, tunda hili linakuwa na nafasi kubwa katika kuimarisha mifupa.