Parachichi ni tunda lenye nyuzinyuzi kwa karibu asilimia 13 ambazo ni sawa na kiwango cha asilimia 54 unachotakiwa kula. Je bado huoni umuhimu wa tunda hili? Anza kula ili uboreshe mmeng’enyo wako wa chakula sasa.
Ni muhimu kwa wajawazito
Kuwepo kwa kiasi kikubwa cha folate, potasiamu, Vitamini C na B6 ambazo ni muhimu kwa ajili ya afya na ukuaji wa mtoto; kunalifanya tunda la parachichi kuwa na umuhimu mkubwa kwa wajawazito.
Huboresha afya ya ubongo
Madini ya kopa yanayopatikana kwenye parachichi kwa zaidi ya asilimia 19 yana nafasi kubwa sana katika kuufanya ubongo ufanye kazi vyema.
Huboresha ufyonzwaji wa virutubisho
Baadhi ya virutubisho hufyonzwa kunapokuwa na mafuta (fat soluble); virutubisho hivyo ni kama vile vitamini A, E, D na K.
Huboresha ufyonzwaji wa virutubisho
Baadhi ya virutubisho hufyonzwa kunapokuwa na mafuta (fat soluble); virutubisho hivyo ni kama vile vitamini A, E, D na K.
Huongeza nguvu za mwili
Miili yetu inategemea sana wanga, protini na mafuta ili kupata nguvu. Ni wazi kuwa sasa unafahamu kuwa tunda la parachichi ni chanzo kikubwa cha virutubisho hivi vitatu.
Naamini sasa hutopuza tena tunda la parachichi kwani umefahamu faida tele za tunda hili. Parachichi ni tunda linalopatikana kwa urahisi bila gharama kubwa ikilinganishwa na matunda mengine kama vile tofaa (apple).
Fanya matunda kuwa sehemu ya mlo wako sasa hasa tunda la parachichi ili uwe na afya njema.