Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hivi karibuni, Mamlaka ya Kenya ya viwango (kebs) ilinyang'anya makampuni ya utengezaji wa Siagi ya karanga inayotumiwa zaidi kupakwa kwenye mikate kutokana na hofu kuwa ilikuwa na sumu kuvu.
 
Madaktari na wataalamu wa chakula waliohojiwa katika taarifa ya uchunguzi ya runinga walisema kuwa baadhi ya watu walikufa kutokana na ulaji wa unga huo unaodaiwa kuwa na sumukuvu.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Kebs alifichua kuwa Wakenya wamekuwa wakila ugali wenye sumu tangu mwaka 2008, huku serikali ikiwa na uelewa fika wa hilo.
 
"Nina uhakika wa zaidi ya 100% kwamba inawaathiri watu na kwamba katika kipindi cha miaka 10 hadi 15 tutakuwa pia na visa vingi vya saratani kokana na mahindi ," Mkurugenzi aliiambia kamati ya bunge la Kenya.
 
Kutokana na hayo Wakenya wameingia katika mtandao wa habari wa kijamjii wa Twitter kupitia hashtag #WhiteAlert huku wakiitaka serikali iwakamate maafisa wanaohusika na kuhakikisha viwango vya usalama wa chakula nchini humo.
 
Tanzania ikiwa ina matumizi ya nafaka kwa kiwango kikubwa Afrika mashariki, vyakula ambavyo vinaweza kuambukizwa sumu kuvu ni kama vile mahindi na unga wake, karanga na mazao yanayotokana na karanga, muhogo.
 
Sumu kuvu inatokana na fangasi ambayo inayoota kwenye mbegu za nafaka, hutokea pale ambapo nafaka ikiwa imetunzwa vibaya.
 
Sumu hiyo mara nyingi husababisha kansa ya ini na inaweza kusababisha vifo vya watu kwa pamoja na kama watu wakila chakula hicho kwa pamoja basi wote wanaweza kuathirika.
 
Mtaalamu wa masuala ya Afya na mwandishi kutoka nchini Tanzania anasema kuwa Sumu kuvu ni tatizo kubwa nchini Tanzania, utafiti uliofanyika mwaka 2012 uliangazia taifa zima na kuonyesha jinsi sumu hiyo inaweza kuathiri chakula kwa kiwango kikubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…