Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hukuwezesha kuhisi njaa
Kuna watu huwa wanashindwa kula vizuri kwa sababu huwa hawahisi njaa vyema. Njia moja wapo ya kupata njaa ambayo itakusababisha ule vyema, ni kufunga kula.
 
Huboresha utendaji kazi wa ubongo
Kufunga kula kunachochea uzalishaji wa protini ya brain-derived neurotrophic factor (BDNF) ambayo ni muhimu sana katika ukuaji, afya na utendaji kazi wa seli za fahamu za ubongo (neurons)
 
Huwezesha kujizalisha upya kwa seli
Seli hukua na kuchakaa au hata kufa kwenye mwili wa binadamu. Kama ilivyo kwa kinga mwili, utafiti unaonyesha kuwa unapofunga mwili huzalisha seli mpya ili kujiaanda au kukabili badiliko lolote linaloweza kutokea.
 
Huboresha afya ya moyo
Watafiti wa afya wanaeleza kuwa kufunga kula kunasababisha mishipa ya moyo na misuli kufanya kazi vyema.
 
Husaidia Kutawala umbo la mwili na mwonekano
Njia nzuri ya kutawala umbo au mwonekano wako ni kwa kutawala kile unachokula. Hii ndiyo sababu walimbwende au warembo hujizuia sana kula hovyo ili wasije wakaharibu mwonekano wao.
 
Huokoa pesa
Hii ni faida ambayo siyo ya kiafya lakini inatokana na kufunga. Kama umezoea kununua chakula, mara ufungapo utaokoa pesa nyingi ambazo ungezitumia kwa ajili ya kula.
 
Naamini hii ndiyo sababu hata watu wenye bajeti ngumu hupunguza milo ya chakula ili waokoe pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…