Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pia utafiti uliofanyika umebaini kuwa kutokupumzika huongeza kiasi fulani cha protini kwenye ubongo ambacho huchangia katika kutokea kwa maradhi ya Alzheimer (Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu).
 
Huondoa hatari ya kupata kiharusi
Kiharusi ni ugonjwa unaosababishwa na kupasuka kwa mishipa midogo ya damu kwenye ubongo; hili husababisha damu kuvuja ndani ya ubongo
 
Utafiti uliofanyika umebaini kuwa uchovu hasa ule unaoambatana na msongo wa mawazo, unaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa inayopeleka damu kwenye ubongo na kisha kusababisha ugonjwa wa kiharusi.
 
Hivyo basi, unapopata muda wa kupumzika unaupa moyo wako nafasi ya kupunguziwa mzigo wa kusukuma damu kwa kasi, ambao umeubeba wakati ulipokuwa unafanya shughuli mbalimbali
 
Huongeza hamasa ya utendaji
Nani anapenda kufanya kazi akiwa amechoka? Naamini hakuna. Kupata muda wa kutosha wa kupumzika kutakuwezesha kujisikia vizuri na kuwa tayari kutekeleza majukumu yaliyoko mbele yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…