Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mchezaji wa Denmark Christian Eriksen anakaribia kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wake, huku Tottenham sasa wakiangalia walengwa wengine lakini Brentford wana matumaini ya kumnunua tena mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Fabrizio Romano)
 
Beki wa Manchester United Brandon Williams, 21, hana mahitaji ya ziada Old Trafford na anaweza kupatikana kwa £10m msimu huu wa joto. (Mail)
 
Leeds wamewatambua kiungo wa RB Leipzig na Marekani Tyler Adams, 23, na kiungo wa kati wa RB Salzburg kutoka Mali Mohamed Camara, 22, kama mbadala wa nyota wa Uingereza Kalvin Phillips, 26, ambaye anaonekana kukaribia Manchester City. (Mail)
 
Chelsea huenda wakamuongeza mshambuliaji wao wa Ujerumani Timo Werner, 26, katika mkataba wa kubadilishana mlinzi wa Juventus na Uholanzi Matthijs de Ligt, 22. (Sky Sports)
 
Mshambulizi wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo, 37, ilikuwa mojawapo ya mada zilizojadiliwa wakati mmiliki mpya wa Chelsea Todd Boehly alipokutana na wakala wa mchezaji huyo Jorge Mendes wiki iliyopita. (The Athletics Usajili unahitajika)
 
Manchester United wanazidi kuwa na uhakika wa kumpata mchezaji Frenkie de Jong, huku ada ya maafikiano ya takriban £69m kufikiwa na Barcelona kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi, 25. (Goal).
 
Hata hivyo, Manchester United wanakabiliwa na tishio la kutumbukia katika deni la £1bn ikiwa wataendelea na mipango ya kuendeleza upya Old Trafford. (Mirror)
 
Porto wanatarajia Liverpool kuimarisha nia yao ya kumnunua winga wa Ureno Otavio, 27, wiki hii baada ya kukataa ofa ya pauni milioni 26 kutoka Leeds United. (Mirror)
 
Roma wanataka kumsajili Ronaldo na kumuunganisha na bosi wake wa zamani katika klabu ya Real Madrid, Jose Mourinho. (Retesport - kwa Kiitaliano)
 
Arsenal wanatazamiwa kuongeza juhudi zao za kumsajili mshambuliaji wa Leeds na Brazil Raphinha, huku klabu hiyo ya London ikifikiriwa kuwa inapewa nafasi kubwa ya kufunga mkataba wa kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (The Athletic -usajili unahitajika)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…