Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kawaida maumivu makali ya tumbo hasa kwa mimba kubwa ya miezi zaidi ya mitano au mimba ndogo kama mwezi mmoja, basi kuna uwezekano mkubwa kondo imeanza kujiondoa kwenye kizazi kwa mimba kubwa au mimba ndogo imeshindwa kuendelea kukua na moja kwa moja hiyo inaweza kuwa dalili ya kuwa mimba imeharibika.
 
Kila mtu aliye mjamzito anategemea mimba iwe inakua kila siku na iwe kubwa kulingana na umri unavyozidi kwenda mbele, ikiwa mimba iko vilevile kwa miezi kadhaa, yaani haikui au ukubwa wa tumbo haubadiliki ujue kwamba mimba hiyo imeharibika, ili kupata uhakika wahi hospitali kupimwa.
 
Mjamzito akitokwa na damu nyingi sehemu za siri ni dalili kwamba mimba imeanza kuachia na mlango wa uzazi umeanza kufunguka, na hiyo inaashiria kwamba kuna mambo mawili yameshatokea kwanza inawezekana mtoto ameshafia tumboni au bado hajafa, lakini kama damu imetoka kwa wingi inaashiria kuwa mtoto huyo aliye tumboni atakufa tu.
 
Mara kwa mara mwanamke akiwa na ujauzito anakuwa na dalili nyingi kama vile kuwa na kichefuchefu, kukosa hamu ya kula baadhi ya vyakula, kutapika, kulamba vitu vichachu kama vile limao, ndimu, wengine hula udogo na wengi hubadilika sana tabia, hivyo basi dalili zote hizo za mimba zikisimama ghafla basi ujue mimba imeharibika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…