Kutembea haraka
Njia rahisi ambayo imethibitika kuweza kumuondolea mtu hali ya kutokujiamini ni kutembea kwa mwendo wa haraka. Haipendezi unapokuwa njiani kutembea kama mgonjwa, uliyechoka. Ukiwa hivyo ni rahisi sana kuwafanya watu wakukodolee macho ambayo yatakufanya wewe uhisi tofauti. Utemebeaji wa haraka una faida nyingi, lakini kubwa kabisa ni kuwafanya watu wengine wakuone wewe ni mtu wa kazi usiyetaka kupoteza muda wako, mtu makini na mwenye mipamgo. Kitaalamu mwendo unaoruhusiwa ni wa asilimia 25, usizidi sana kiasi cha kuonekana kamaunakimbia.