Je! Ushawahi kutokewa na hali hii?
umelala halafu ghafla unashtuka
usingizini kwa mguvu nyingi kama
umepigwa na shoti ya umeme na akili
inakurudi ghafla huku mapigo ya
moyo yakikuenda mbio? Na hali hii
ikakutokea pasipo hata kuota ndoto
yoyote?
Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa
kwa hiari ambayo huwatokea watu
mara tu wamejinyoosha kitandani na
kupitiwa na usingizi, mwili
hutetemeshwa na kusukumwa kwa
nguvu na mtu hushtuka katika hali
kama vile kapigwa na shoti ya umeme.
Wanasayansi wanatuambia kua, pale
tu unapopata usingizi kiwango cha
upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya
moyo nayo taratibu yanapungua,
misuli inatulia kwa ku-relax,
Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii
kama ni DALILI ZA KIFO (brain’s misinterpretation of muscle
relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa
kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu hali ambayo humfanya mtu kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida.
Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezekakwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema haraka haraka na wakati mwingine mtu hutokwana jasho jingi.
Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia kukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kunatatizo gani?