Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Utafiti uliofanyika huko India ulibaini kuwa watu wengi waliokufa kutokana na maradhi ya figo waliishi katika mazingira yenye sumu za kuulia wadudu au kula vyakula vyenye mabaki ya sumu hizo.
 
Kutokana na watu wengi kutumia dawa za kuulia wadudu bila kuvaa vifaa vya kujikinga, wengi huvuta sumu zilizoko kwenye dawa hizo na kusababisha kuathiri mfumo wa upumuaji hasa mapafu.
 
Kama ilivyo kwenye swala la kuathiri mfumo wa upumuaji, watumiaji wengi wa dawa za kuulia wadudu hawakingi ngozi zao kwa mavazi au vifaa maalumu vinavyoepusha athari za dawa hizo kwenye ngozi zao.
 
Naamini umeona jinsi ambavyo dawa za kuulia wadudu — viwatilifu zinavyoweza kuathiri afya ya binadamu ikiwa hazitatumiwa kwa uangalifu na kwa kufuata kanuni muhimu za matumizi yake.
 
Data za mauzo ya simu janja katika robo ya kwanza ya mwaka 2022 (Januari - Machi) imetoka, kampuni ya Samsung imeongoza kwa kuuza simu nyingi zaidi huku ikifuatiwa na Apple.

Orodha kamili;

1. Samsung - 22.4%

2. Apple - 18.0%

3. Xiaomi - 12.7%

4. Oppo - 8.7%

5. Vivo - 8.1%

6. Kampuni zingine (Tecno, Google Pixels, Huawei etc.) - 29.1%
 
Sifa za wanawake wa kichaga;

  • Wazuri kisura
  • Wasomi
  • Wakipenda, wanapenda kweli
  • Hawako romantiki kwenye uhusiano 😒
  • Wachapakazi na wanapenda kujitegemea
  • Wavumilivu mno!
  • Wanapenda hela
 
Utamaduni: Ndoa za kisukuma zinaruhusu ndoa za mitara (mke zaidi ya mmoja). Kwa kawaida wasukuma huoa kwa mahari ya ng'ombe kati ya 7 mpaka 20, hii ni kawaida lakini mahari inaweza kuwa ng'ombe 25 mpaka 70 pale atakapokuwa anaozeshwa binti mweupe.
 
Wanasayansi wanashauri wanawake kupata muda mwingi zaidi wa usingizi kwa kile wanachodai kua ubongo wao ni tata zaidi kuliko wa Wanaume. Ubongo wa Wanawake unafanya kazi nyingi zaidi ukilinganishwa na Wanaume.
 
Saikolojia: Watu wanaopenda kulalamika/kuponda kuhusu mambo ambayo watu wengine wanafanya, kwa kiasi kikubwa ndicho pia na wao wanakifanya au wanatamani kufanya.
 
Wasukuma ndio kabila kubwa zaidi kwenye mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu na Tabora. Wanasifika kwa upole, ukarimu na kutokuwa wabahili, wakipenda wamependa kweli.
 
Homo Erectus waliweza kuishi duniani kwa takribani miaka milioni 1.9, na ndio kipindi katika historia ya maisha ya mwanadamu kilicholeta mabadiliko zaidi. Homo Sapiens ambao ndio sisi 😒 mpaka sasa tupo duniani kwa miaka zaidi ya 300,000 tu.
 
Moja ya faida ya kuoga maji ya baridi ni husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kuna Fat Cells zinapatikana zaidi maeneo ya shingo na kwenye mabega huwa zinayeyuka kirahisi zaidi pale mwili unapokua kwenye hali ya ubaridi.
 
Tafiti: Kuoga maji ya baridi mara kwa mara kwa mwanaume husaidia kuboresha uimara wa mbegu. Maji ya baridi yanaongeza kiwango cha homoni ya testestorone ambayo hufanya kazi muhimu kwenye maendeleo ya ukuaji na uimara wa mbegu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…