Meneja wa Arsenal Arteta amethibitisha kwamba mlinzi William Saliba yuko kwenye mipango yake. Vilabu kadhaa vya Ufaransa na Hispania vinamtolea macho kinda huyo mfaransa.
Brighton imekataa ofa ya Manchester City kwa ajili ya mlinzi Marc Cucurella. Ofa ya £30m inaonekana kuwa ndogo, Brighton wanataka £50m. Mazungumzo yanaendelea (David Ornstein)
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Thomas Muller amekataa uwezekano wa kujiunga na Arsenal akimjibu mmoja wa mashabiki wa Gunners aliyemuuliza kama anaweza kujiunga na wakali hao wa London.
Video imesambaa leo ikimuonyesha Mjerumani huyo mwenye miaka 32 aliyetwaa mataji 11 ya ligi kuu ya Ujerumani akimjibu mshabiki huyo wakati akisaini vitabu vyao 'hapana, hapana'.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.