Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Fisi: 80% ya chakula chao hukipata kwa kufanya mawindo, 20% hupata kwa kula mizoga au kupora kutoka kwa wanyama wengine kama Simba, Duma baada ya kuwinda.
 
Garry Harrington kutoka jimbo la Oregon, Marekani mwaka 2012 alihukumiwa kifungo cha siku 30 gerezani na kutozwa faini ya Tzs 3,473,930/= Kwa kosa la kukusanya maji ya mvua bila kibali. Katika jimbo hilo mvua inatajwa kuwa mali ya serikali, hivyo inabidi uwe na kibali kama unataka kukusanya maji yake.
 
Kabila la Kreung linapatikana nchini Cambodia, Baba huwajengea vijumba maalumu mabinti zao pindi wanapofika umri wa kuolewa kwaajili ya kukutania kimwili na wanaume mbalimbali mpaka pale binti atakapopata anaemfaa. Kreung' wanaamini hiyo ndio njia sahihi ya kumpata Mume.
 
Mbwa wanaotumika Jeshini mara nyingi huwa na cheo cha juu zaidi kuliko anaemtunza (handler), lengo ni kupunguza uwezekano wa kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji na huyo Handler wake. Akifanya hivyo kosa linakua ni kushindwa kumheshimu Mkuu wake kikazi!
 
Tafiti: Kuoga maji ya baridi mara kwa mara kwa mwanaume husaidia kuboresha uimara wa mbegu. Maji ya baridi yanaongeza kiwango cha homoni ya testestorone ambayo hufanya kazi muhimu kwenye maendeleo ya ukuaji na uimara wa mbegu.
Sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…