Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Huboresha metaboli
Embe ni tunda lenye nyuzinyuzi kwa kiasi kikubwa. Nyuzinuzi zinahitajika sana katika kufanya mchakato wa metaboli (mwili kutumia vrutubisho kujipa nguvu) kwenda vizuri.
 
Huboresha afya ya macho
Kula embe kutakunufaisha kwa kulinda macho yako dhidi ya kudhoofu kwa misuli ya macho. Embe ni chanzo kizuri cha vitamini A ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho.
 
Huweza kuzuia saratani
Tunda la embe limesheheni kemikali kama vile methylgallat, astragalin, isoquercitrin, fisetin, quercetin na gallic acid ambazo kwa pamoja zinazuia kutokea kwa maradhi ya saratani. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa pectin inayopatikana kwenye maembe huvuruga utendaji kazi wa galectin 9 ambayo hupatikana kwenye seli za saratani
 
Hukabili shinikizo la damu mwilini
Madini ya potasiamu yanayopatikana kwenye embe huasidia dosari zinazosababishwa na madini ya sodiamu katika damu. Potasiuam hurekebisha nguvu ya msukumo wa damu (blood pressure) na kuufanya uwe wa kawaida
 
Huongeza alkaline mwilini
Asidi za tartaric na malic inazopatikana kwenye embe huongeza kiwango cha alkaline mwilini. Alkaline ni muhimu kwani husaidia kuzuia maradhi ya figo pamoja na udhaifu wa mifupa. Alkaline husaidia pia kuwezesha usafirishaji wa oksijeni katika mwili mzima.
 
Hutumika kama kipodozi cha nywele
Kwa kuchanganya ujiuji wa embe, yai pamoja na kijiko kimoja cha asali, na yogurt; unaweza kupata kipodozi kizuri kwa ajili ya nywele zako. Paka mchanganyiko huu na subiri kwa muda wa dakika thelathini kabla ya kuosha nywele zako.
 
Back
Top Bottom