Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Asilimia 10 ya maisha ni jinsi unavyoyapata, na asilimia 90 jinsi unavyoyakubali.” -Irving Berlin
 
Watu wanapenda kujua ni nini kinachowasukuma wengine kufanya vizuri zaidi. Hapa kuna baadhi ya 'maisha ndiyo unayoyafanya kuwa nukuu na misemo ambayo ni muhimu kwa kila mtu.
 
Ripoti ya Chama cha Wanasheria, shirika la kitaaluma la mawakili nchini Uingereza, limesema kuwa chip ya kompyuta inaweza kupandikizwa kwenye akili za mawakili, jambo ambalo linaweza kupunguza gharama za kesi na kupunguza idadi ya mawakili kutatua kesi ngumu.
 
Ripoti hiyo, 'Neuroteknolojia, Sheria na Taaluma ya Sheria', iliandaliwa na Dk Alan McKay kwa ombi la Chama cha Wanasheria cha Uingereza na Wales.
 
Katika ripoti hii, Dk. McKay, anayehusishwa na Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Sydney, Australia, anajadili faida zinazoweza kupatikana za kutumia akili bandia katika taaluma ya sheria au sekta ya sheria.
 
Watetezi wa kuanzisha teknolojia ya neva (neurotechnology) kwa wanasheria wanasema kuwa wateja wa makampuni au wateja wa biashara wanashinikiza chip kama hiyo, wakisema inaboresha utendakazi.
 
Kwa hivyo, mawakili wanaotoza £1,500 kwa saa watalazimika kutoza ada zao kulingana na 'vitengo vya malipo vinavyoweza kutozwa', yaani, muda waliotumia kufanyia kazi au kufikiria kuhusu kesi.
 
Nimetumia muda gani? Kana kwamba watalipwa kulingana na mita iliyounganishwa na ubongo badala ya muda wa kwenye saa.
 
Chama cha Wanasheria, ambacho kinahusika na masuala ya kitaaluma ya wanasheria nchini Uingereza na Wales, kilisema katika ripoti iliyochapishwa hivi karibuni kwamba chip ya ubongo kama hiyo itakuwa 'iPhone ya siku zijazo' kwa sekta ya sheria.
 
Hakutakuwa na haja ya timu kubwa ya mawakili kushughulikia kesi ngumu, lakini Wakili mkubwa mwenye chip ataweza kupembua maelfu ya nyaraka na maelezo kuhusiana na mambo mbalimbali ya kesi hiyo kwa muda mfupi sana na kutengeneza hoja zake kuu namaoni.
 
Ingawa makampuni ya kimataifa yana ada kubwa ya uanasheria kama sehemu ya biashara, kupunguzwa kwa gharama za kisheria kwa msaada wa teknolojia hakika kutavutia watendaji wakuu wa makampuni haya.
 
Back
Top Bottom