Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kufanya mambo yako kwa malengo, ni wazi kuwa mtu yeyote anayejitambua ni lazima atafanya mambo yake kwa kusudi au malengo maalum na hivyo kumuhakikishia kutimiza ndoto zake.
 
Kufanya mambo yake kwa kujiamini, hii niiweke wazi kwa kusema kuwa kwa mtu yeyote anayejitambua ni lazima atakuwa na sifa yakujiamini popote pale atakapo kuwepo na hivyo kumuongezea nafasi ya yeye kufanikisha lile alifanyalo bila kuwa na yoga au hofu yoyote ile.
 
Sifa ya uongozi; ukubali au ukatae ila ni ukweli usiopingika kuwa asilimia Kubwa ya wanao waongoza wengine huwa ni watu wanaojitambua, na hiyo ni kwasababu huwezi kumuonesha njia mwenzako ilihali wewe binafsi huifahamu vizuri hiyo njia, hivyo kujitambua hutupatia sifa ya uongozi kwa wengine.
 
Kujitambua kunaleta Hamasa, hii nikiwa na maana ni vigumu sana kwa mtu asiyejitambua kushawishika Kufanya jambo fulani, ila ni rahisi sana kwa mtu anayejitambua kuhamasika (kujihamasisha) Kufanya jambo Fulani.
 
Hivyo basi kwa kusema hayo machache ningependa kukuhamasisha uamke sasa na kuanza kujitambua ni kipi has a unataka maishani mwako na uanze kukifanya sasa pasipo kuwa na hofu yoyote ile.
 
1661181244515.png
 
Back
Top Bottom