Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye biashara na huduma nyingi mteja huchukuliwa kama kitu kisicho na nafasi wala umuhimu wowote
 
Lakini ukweli ni kuwa mteja ni msingi muhimu sana katika kufanikiwa kwa huduma au biashara yoyote ile.
 
Kumbuka biashara yoyote isiyozingatia kutoa huduma nzuri kwa wateja wake itapoteza wateja na hatimaye itakufa
 
Kwa kutambua umuhimu wa kutoa huduma nzuri kwa wateja karibu nikushirikishe mambo 10 ambayo unapaswa kuyazingatia ili kutoa huduma nzuri.
 
Elewa hitaji la mteja

Kamwe huwezi kumhudumia mteja vizuri bila kufahamu hitaji lake. Mara mteja anapofika katika biashara yako hakikisha unafahamu na kuelewa vyema anahitaji nini kabla ya kumhudumia.
 
Jitosheleze kihuduma

Kabla ya kuamua kutoa huduma yoyote kwa mteja hakikisha unajitosheleza katika kutoa huduma .
 
Hakikisha vitendea kazi vyote kama vile bidhaa, mifumo, chenji na maarifa na ujuzi wa kutoa huduma husika unavyo vya kutosha ili uweze kutoa huduma nzuri kwa mteja.
 
Si jambo sahihi mteja kuja kwenye biashara yako kisha unaanza kumwambia kauli kama vile: Ngoja nikakubadilishie hii bidhaa pale, ngoja nikaombe chenji pale, ngoja nikaulize bei ya hiki kitu kwa jirani, ngoja nimpigie bosi anieleze jinsi ya kutoa huduma hii n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…