Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mthamini mteja kuliko pesa

Mara kadhaa nimekuwa nikisisitiza kuwa pesa ni ujira anaopewa mtu baada ya kutatua tatizo la mteja
 
Hata hivyo, jambo la kusikitisha ni kuwa wafanyabiashara wengi hutazama zaidi kupata pesa kuliko kumridhisha mteja kwa huduma nzuri kwanza.
 
Hii ndiyo sababu wafanya biashara hupanga bei hovyohovyo au hata kwa kuiga bila kumfikiria mteja zaidi. Wafanya biashara wanaothamini zaidi pesa wao hufanya jitihada sana kuhakikisha mteja analipia bidhaa au huduma hata kama atafanya hivyo kwa shingo upande au akilalamika
 
Ukitazama kwa makini pia utabaini kuwa hii ni moja ya sababu inayofanya baadhi ya wafanya biashara kuuza bidhaa bandia au kwa njia ya ujanja ujanja ili tu wapate pesa.
 
Jifunze lugha nzuri kwa mteja

Suala la lugha duni kwa mteja ni tatizo kubwa sana katika biashara nyigi za sasa.
 
Kwenye biashara nyingi wateja hujibiwa kwa mkato, mkato au hata kukejeliwa na watoa huduma kwani wanaonekana hawana thamani bali wenye thamani ni wafanya biashara/watoa huduma
 
Ikiwa unataka kufanikiwa kwenye biashara yako ni lazima uhakikishe umetoa kauli nzuri kwa mteja. Hakikisha mambo yafuatayo katika suala hili,
 
Mshukuru na mkaribishe mteja kuja wakati mwingine. Unaweza pia kumjulisha kuhusu huduma nyingine zilizopo ili atakapozihitaji wakati mwingine afahamu atakapozipata.
 
Pasipo shaka ukizingatia mambo tajwa hapo juu utatumia mbinu ya kauli nzuri kwa mteja ili kufanikisha utoaji wa huduma bora.
 
Kuwa mwaminifu
Kuna msemo usemao “uaminifu ni mtaji” Ndio uaminifu ni mtaji muhimu sana katika kufanikisha suala la kutoa huduma nzuri kwa mteja hasa katika dunia na kipindi hiki ambacho watu wengi siyo waaminifu.
 
Wewe kama mfanya biashara au mtoa huduma hakikisha unazingatia mambo yafuatayo katika kutoa huduma kwa uaminifu:
 
Back
Top Bottom