Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuwa mwaminifu juu ya mali na fedha za mteja. Iwapo mteja atasahau au atazidisha fedha hakikisha unamrejeshea fedha au mali yake.
 
Unapobaini mteja amepata tatizo kama vile kupata huduma au bidhaa yenye dosari, hakikisha unatafuta njia ya kumsaidia na si kujitetea kuwa mali ikishauzwa hairudishwi au kubadilishwa.
 
Hakikisha unatoa huduma na bidhaa unazotozitangaza na kuzielezea kuwa zipo kwenye biashara yako. Kwa mfano siyo sawa kusema unauza mchele safi lakini ukauza mchele uliojaa chuya au mawe. Au kujinasibisha Kuwa unatoa huduma 10 kumbe zinazopatikana ni mbili tu.
 
Pasipo shaka ukizingatia haya utatumia mbinu ya uaminifu katika kuhakikisha unatoa huduma nzuri kwa wateja wako.
 
Jali muda wa mteja
Kwa hakika hakuna mteja anayependa kupoteza muda wake wakati wa kutafuta huduma au bidhaa.
 
Uwapo katika biashara hakikisha unatengeneza mfumo mzuri wa utoaji huduma ambao hautompotezea mteja muda.
 
Ikiwa biashara yako inahudumia wateja kwa wingi andaa utaratibu wa kuajiri watoa huduma zaidi ili kupunguza foleni kwa wateja.
 
Pokea maoni na mrejesho
Biashara nyingi hazifahamu umuhimu wa kupokea maoni au mrejesho kutoka kwa wateja, na hii ndiyo sababu si jambo la kawaida kuona biashara nyingi za kiafrika zikipokea mrejesho kutoka kwa wateja.
 
Unapojijengea utaratibu wa kupokea maoni na mrejesho kutoka kwa wateja utabaini changamoto zinazowakabili wateja ili uziboreshe pamoja na kufahamu wateja wanapendekeza au wanahitaji ufanye maboresho gani. Kupitia maoni na mrejesho kutoka kwa wateja utaweza kubaini ikiwa mipango na mbinu zako za mauzo na utoaji huduma kama zina ufanisi au la.
 
Tumia nafasi ya teknolojia
Ulimwengu umebadilika kwa kiasi kikubwa vivyo hivyo pia ulimwengu wa biashara.
 
Kufanya biashara katika ulimwengu huu wa sasa bila kuzingatia nafasi ya teknolojia ni sawa na kufanya kazi gizani.
 
Hakikisha unatumia teknolojia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wateja pamoja na utunzaji wa taarifa zako muhimu za biashara ili biashara iwe na ufanisi
 
Matumizi stahiki ya teknolojia yatakuwezesha kutoa huduma nzuri kwa wateja ambayo wataifurahia na kuona thamani halisi ya pesa yao
 
Tumia nafasi ya fidia na kuomba msamaha
Siyo kila mara mambo yote yataenda sawa kwa wateja. Ukiwa kama mfanyabiashara anayejali suala la kutoa huduma bora kwa wateja ni lazima uweke utaratibu wa fidia na kuomba radhi pale ambapo jambo fulani halikwenda sawa kwa mteja.
 
Moja kati ya jambo linalo tangaza biashara kama inatoa huduma bora kwa wateja ni namna inavyofanya kazi changamoto zinazokabili wateja wake. Unaweza kufanya yafuatayo:
 
Tengeneza utaratibu wa kupokea na kutatua changamoto za wateja wanaohitaji fidia au matengenezo
 
Ondoa/Boresha bidhaa na huduma zinazoleta changamoto au zinazohitaji fidia na matengenezo kwa wateja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…