Na lau kuwa si Fadhila ya Allaah na Rehma Yake juu yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), bila shaka kundi miongoni mwao lingefanya hima kudhamiria kukupoteza. Na hawazipotezi ila nafsi zao, na hawakudhuru kwa chochote. Na Allaah Amekuteremshia Kitabu na Hikmah na Akakufunza yale ambayo hukuwa unayajua. Na Fadhila za Allaah juu yako daima ni adhimu (na kubwa mno).