Kikosi cha Bush Stars, waliosimama kuanzia kushoto ni Komredi Kipepe (Nahodha), Kepu, Ndondo, Huihui, Kobelo na Mzee Meko. Waliochuchuma kuanzia kushoto ni Mdindifu, Mtwivira, Madenge, Kizibao na Zoba. Hii ilikuwa ni mwaka 1993 dakika chache kabla ya kuwavaa Born Town kwenye uwanja wa Manyasini, na Bush Stars walishinda goli 2 bila zote alitupia kambani Mzee Meko. Na baada ya ushindi timu ilirejea bush na kupokelewa kibabe sana na wanakijiji ikifuatiwa na 'party' bab' kubwa wanakijiji walicheza na kulewa sana ulanzi. Katika sherehe hizo Mzee Meko aliyekuwa nyota wa mchezo kwa kutupia goli zote mbili, alizawadiwa ng'ombe mzima na maziwa yake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.