Na haiwi kwa Muumini amuue Muumini ila kwa kukosea tu. Na atakayemuua Muumini kwa kukosea, basi aachilie huru mtumwa Muumini na atoe diya kwa kuifikisha kwa ahli zake, isipokuwa kama wenyewe watasamehe. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu naye ni Muumini, basi (aliyeua) aachilie huru mtumwa Muumini. Na akiwa ni miongoni mwa watu ambao kuna mkataba baina yenu na baina yao, basi wapewe diya watu wake na aachiliwe huru mtumwa Muumini. Asiyepata, afunge (Swiyaam) miezi miwili mfululizo kuwa ni tawbah kwa Allaah.[23] Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.