myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
✔️✔️Basi mna nini hata mmekuwa makundi mawili kuhusu wanafiki, na hali Allaah Amewageuza (warudie ukafiri) kwa sababu ya waliyoyachuma? Je, mnataka kumhidi ambaye Allaah Amempotoa? Na aliyepotozwa na Allaah basi hutompatia kamwe njia (ya kumhidi).
SawaNa mtakaposafiri katika ardhi basi si dhambi kwenu kufupisha Swalaah mkikhofu kwamba waliokufuru watakushambulieni. Hakika makafiri wamekuwa kwenu ni maadui dhahiri.
🤲🤲Basi hao bila shaka Allaah Atawasamehe. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Kughufuria.
🙏🙏Hakika wale ambao Malaika wanawafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao, (Malaika) watawaambia: Mlikuwa katika hali gani? Watasema: Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi. (Malaika) Watasema: Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni Jahannam, na uovu ulioje mahali pa kuishia!
✔️🤲Ni daraja za vyeo (vya juu) kutoka Kwake na maghfirah na rehma. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
🙏🤲Na anayehajiri katika Njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia kujihifadhi na wasaa (wa kila kitu). Na atakayetoka nyumbani kwake akiwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake, kisha mauti yakamfikia, basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
AiseeHawawi sawa kati ya Waumini wanaokaa (nyumbani), isipokuwa wale wenye udhuru, na kati ya wenye kupigana Jihaad katika Njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao. Allaah Amewafadhilisha kwa cheo wenye kupigana Jihaad kwa mali zao na nafsi zao kuliko waliokaa nyuma. Na wote Allaah Amewaahidi Al-Husnaa (Jannah). Na Allaah Amewafadhilisha wenye kupigana Jihaad kwa ujira mkubwa mno kuliko wanaokaa (nyuma).
🙏🤲Enyi walioamini! Mnapotoka kwenda kwenye Jihaad basi hakikini kila jambo, na wala msimwambie anayekuamkieni kwa As-salaam: Wewe si Muumini kwa sababu ya kutamani mafao yapitayo ya uhai wa dunia na hali kwa Allaah kuna ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa kabla na Allaah Akakufanyieni ihsaan, basi fanyeni uhakiki. Hakika Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi daima wa Khabari za dhahiri na siri.
SawasawaIsipokuwa wale waliokimbilia kupata hifadhi kwa watu ambao kuna mkataba kati yenu na wao, au wale waliokujieni vifua vyao vimedhikika kupigana nanyi au kupigana na watu wao (hao msiwapige). Na lau Allaah Angelitaka, Angeliwasalitisha juu yenu, wakapigana nanyi. Watakapojitenga nanyi na wasipigane nanyi, na wakakuwekeeni amani, basi Allaah Hakukufanyieni njia dhidi yao
SawasawaNa atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni Jahannam, atadumu humo, na Allaah Atamghadhibikia, Atamlaani na Atamuandalia adhabu kubwa mno
✔️✔️Na atakayemuua Muumini kwa kusudi, basi jazaa yake ni Jahannam, atadumu humo, na Allaah Atamghadhibikia, Atamlaani na Atamuandalia adhabu kubwa mno
✔️✔️Na haiwi kwa Muumini amuue Muumini ila kwa kukosea tu. Na atakayemuua Muumini kwa kukosea, basi aachilie huru mtumwa Muumini na atoe diya kwa kuifikisha kwa ahli zake, isipokuwa kama wenyewe watasamehe. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu naye ni Muumini, basi (aliyeua) aachilie huru mtumwa Muumini. Na akiwa ni miongoni mwa watu ambao kuna mkataba baina yenu na baina yao, basi wapewe diya watu wake na aachiliwe huru mtumwa Muumini. Asiyepata, afunge (Swiyaam) miezi miwili mfululizo kuwa ni tawbah kwa Allaah.[23] Na Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote.
AiseeMaisha ni kama zero, Ulipo anzia ndipo unaweza ishia, ikiwa kama hautakua makini na Mipango yako, Zero to zero.
Mungu atulinde🤲🙏Na utapokuwa upo kati yao, ukawaswalisha, basi lisimame kundi miongoni mwao pamoja nawe, na wachukue silaha zao. Watakaposujudu, wawe nyuma yenu (kuwalinda). Na lije kundi jingine ambalo halikuswali, liswali pamoja nawe, nao washike hadhari na silaha zao. Wale waliokufuru wanatamani kama mtaghafilika na silaha zenu na vifaa vyenu wakuvamieni mvamio mmoja. Na wala si dhambi kwenu ikiwa mna maudhiko kutokana na mvua au mkiwa wagonjwa kuweka (chini) silaha zenu. Na mshike hadhari zenu. Hakika Allaah Amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.
Sawa kabisaHakuna kheri katika minong’ono yao mingi isipokuwa anayeamrisha kutoa swadaqa, au mema, au kusuluhisha baina ya watu. Na atakayefanya hivyo kutaka Radhi za Allaah, basi Tutampa ujira mkubwa kabisa.