myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Sawa kabisaKuna muda lazima utambue kua kuna watu wanaweza kubaki moyoni mwako lakini sio maishani mwako
UjumbeMtu mwenye wivu hata ikatokea ukamzidi dhambi. Mara nyingi huwa anachukia sana. Sijui huwa wanashida gani.
✔️✔️Wanaomba Habari mbaya zitokee kwetu watucheke. Ila kila siku zinatokea kwao na tunanyamaza tu.
🤲🤲🤲Unaposkia wanasema acha tuone atafika wapi. Usikate tamaa. Hatma yako haipo kwao. Ipo mikononi mwa Mungu.
Mafanikio.....Aliyekufundisha kuvuka barabara ndio anahitaji leo ugongwe na gari. Binadamu atakuonesha njia ya mafanikio ila haitaji umpite hayo Mafanikio.
SawaJifunze kukaa kimya sio kila mtu yuko upande wako. Wengine wanahitaji wajue mipango yako Ili wakapange mipango Yao.
NakubaliMambo mengine ni bora usiyafahamu ili ubaki kuwa na Amani.
Kuanza upya....Usipende kujihukumu kila wakati. Jisamehe then sahau na uanze upya.
SawasawaKujihukumu kila wakati kutakufanya ushindwe kuendelea mbele.
Nakubali hili piaUsipende kujihukumu kila wakati. Jisamehe then sahau na uanze upya.
Kweli piaMambo ni mawili tu kwa huyo mwanamke wako. Umtunze ama utunziwe. Kwahiyo utachagua mwenyewe.
Lengo uwe sawa.....Anaye kupenda ni yule anaye kuambia ukweli. Hata kama utachukia ila Lengo ubadilike.
SawaBinadamu kukumbushana. Usije kuweka simu mfuko uliouwekea Hela.
🤲🤲Ukiishi kwa kulifatisha neno lake na mafunzo yake hakika utaishi kwa furaha na amani na baraka zake Mungu zitakuwa juu yako.
Ujumbe muhimuUkikielewa kifo, Umeyaelewa maisha, Maisha yamejawa na kwaheri za ghafla sana, tusichoke kujuliana hali,kuombeana na kupendana wakati huu tupo Hai.
🙏🙏Hakuna kikomo cha Mungu kukuinua ikiwa utaendelea kuwa mnyenyekevu mbele yake