Hijja ni mojawapo ya nguzo muhimu za Uislamu. Ni moja ya nguzo tano za dini na ni wajibu kwa kila mtu ambaye ana uwezo wa kuhiji kufanya hivyo angalau moja katika maisha yake.
Kila mwaka wakati huu, mamilioni ya Waislamu kutoka duniani kote husafiri hadi Makka, Saudi Arabia, mahali patakatifu zaidi katika Uislamu, kufanya sherehe hii takatifu.
Kwa ujumla, Waislamu hupendelea kuwazika ndugu zao waliofariki katika makaburi ya karibu ili waweze kuwatembelea na kuwaombea dua. Mara nyingi, linapokuja suala la watu wanaofariki mbali na nyumbani, wapendwa wao hutumia gharama nyingi ili tu kurejesha mwili wa mpendwa wao kwa mazishi.
Kwa ujumla, Waislamu hupendelea kuwazika ndugu zao waliofariki katika makaburi ya karibu ili waweze kuwatembelea na kuwaombea dua. Mara nyingi, linapokuja suala la watu wanaofariki mbali na nyumbani, wapendwa wao hutumia gharama nyingi ili tu kurejesha mwili wa mpendwa wao kwa mazishi.
Kwa kweli, ni fursa nzuri kufariki katika nchi takatifu. Hata wazazi wa marehemu, ingawa wanahisi uchungu juu ya kifo cha mpendwa wao, wanakubali maumivu haya kutokana na imani kwamba ni baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Zaidi ya hayo, Uislamu unaagiza kwamba ni vizuri kuwazika watu waliokufa haraka iwezekanavyo baada ya kifo chao, kwa kawaida Muislamu aliyefariki huzikwa ndani ya saa 24 baada ya kifo.
Imam Nurudeen wa Anoda, ambaye amekwenda kushiriki ibada ya Hija mara kadhaa, ameiambia BBC Idhaa ya Pidgin kwamba kuna makaburi kadhaa ambapo mahujaji wanaofariki wakati wa Hija wanaweza kuzikwa.
Baadhi ya makaburi yanayojulikana zaidi ni pamoja na Jannat Al-Mala huko Makka, Jannat Al-Baqi huko Madina, Makaburi ya Al-Adl, Makaburi ya Mashahidi wa Al-Haram, Makaburi ya Al-Rabway na Makaburi ya 'Arafat.
Mnamo mwaka wa 2015, wakati zaidi ya mahujaji 2,000 walipofariki katika mkanyagano uliotokea Mina, mamlaka ya Saudia ilisema walikuwa wametayarisha makaburi ya kutosha katika maeneo ya makaburi sita ili kuwazika waathiriwa.
Sulaiman Aliyu, mfamasia katika Hospitali ya mafunzo ya Ahmadu Bello huko Zaria, katika jimbo la Kaduna, anaameiambia BBC taratibu za kuwazika mahujaji wanaofariki wakati wa Hijja.
Anasema: "Kwanza kabisa, yote inategemea mahali ambapo mhujaji alifariki. Huenda huenda akafariki katika hospitali au zahanati ya Nigeria, kwa vile NAHCON (Tume ya Kitaifa ya Hija ya Nigeria) ina kliniki yake katika nchi takatifu, au anaweza kufia katika chumba chake cha hoteli.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.