Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Basi yule ambaye Allaah Anataka kumhidi, Humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule ambaye Anataka kumpotoa, Hufanya kifua chake kiwe na dhiki chenye kubana kama kwamba anapanda kwa tabu mbinguni. Hivyo ndivyo Allaah Anavyojaalia adhabu (au Anavyowasalitishia shaytwaan) kwa wale wasioamini.
 
Na Siku Atakapowakusanya wote (Allaah Atasema): Enyi hadhara ya majini! Kwa yakini mmewapoteza wanaadamu wengi sana. Na watasema marafiki wao wandani katika wanaadamu: Rabb wetu! Tulinufaishana sisi kwa sisi, na (leo) tumefikia muda wetu ambao Umetupangia. (Allaah) Atasema: Moto ndio makazi yenu, mtadumu humo, isipokuwa Atakavyo Allaah. Hakika Rabb wako Ni Mwenye Hikmah wa yote, Mjuzi wa yote.
 
Enyi hadhara ya majini na wanaadamu! Je hawajakufikieni Rusuli miongoni mwenu wanakusimulieni Aayaat Zangu na wanakuonyeni kukutana na Siku yenu hii? Watasema: Tumeshuhudia dhidi ya nafsi zetu. Na uliwaghuri uhai wa dunia, na wameshuhudia dhidi ya nafsi zao kwamba hakika wao walikuwa ni makafiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…