Tai hupenda dhoruba. Mawingu yanapojikusanya, tai hufurahia, tai huutumia upepo wa dhoruba kupanda juu zaidi. Mara tai anapokutana na upepo wa dhoruba, huitumia dhoruba kupanda juu ya mawingu. Hii humpa tai fursa ya kuelea na kupumzisha mabawa yake. Wakati huo ndege wengine hujificha kwenye matawi na majani ya miti.
MAANA: Kabiliana na changamoto zako uso kwa uso huku ukitambua kuwa zitakuacha ukiwa imara na bora kuliko ulivyokuwa. Tunaweza kutumia dhoruba za maisha kupanda ngazi za juu zaidi. Wapambanaji huwa hawaogopi kufika hatua za juu zaidi. Wapambanaji huwa hawaogopi changamoto, zaidi huzikabili na kuzitumia kwa faida.