Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matumizi ya muda mrefu ya paracetamol au acetaminophen yanaweza kusababisha madhara makubwa katika figo na Ini.
 
VEGA ( SILDENAFIL): viagra au vega ni dawa inayotumika sana miongoni mwa wanaume kwa lengo la kuongeza uwezo wao wa kufanya mapenzi ( sex)
 
Matumizi ya dawa hizi bila ushauri wa daktari nihatari kwani inaweza pelekea matatizo ya moyo na hata kifo cha ghafla
 
ASPIRIN: aspirin ni dawa muhimu sana lakini inaweza kuwa hatari ikitumiwa kiholela kwa sababu sio salama kwa kila mtu.
 
Dawa hii inajulika kwa ubora wake wa hali ya juu ya kutuliza maumivu na wakati mwingine hutumiwa kutuliza homa
 
Inaweza kusababisha chakula kisisagike vizuri hali ambayo inaweza kumsababishia mtu kupatwa na vidonda vya tumbo.
 
Inaweza kuwafanya watoto kupata na ugonjwa hatari unaojulikana kama (Reye syndrome) ambayo inaweza kuathiri (ini au ubongo).
 
NB: Usimpatie mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 16 asprin bila ushauri wa daktari
 
DICLOFENAC: Matumizi ya kiholela ya dawa za kupunguza maumivu na uvimbe huchangia ongezeko la hatari ya kupata maradhi ya moyo.
 
Dawa kama vile Ibruprofen, Naproxen na Diclofenac ndizo dawa hutumiwa sana kupunguza maumivu na uvimbe.
 
DICLOPAR: Sikuhizi watu wakimeza Paracetamol wanadai kwamba haitulizi maumivu na kukimbilia diclopar.
 
Nidawa hatari sana kwa afya yako, endapo utaitumia bila ushauri wa daktari, Ukitumia dawa hihi mara kwa mara inaweza pelekea Matatizo ya mifupa na joints hapo badae.
 
FLAGYL (METRONIDAZOLE),, Dawa nyingine ambayo inatumiwa vibaya inafahamika kama flagyl.
 
Baadhi ya watu huzinunua bila maelekezo ya dakatari. Wapo wanawake wameigeuza hii dawa P² au za kutolea mimba Nihatari sana kwa afya kutumia dawa kwa kutegemeana faida kwenye side effects...Hapo nikujimaliza mwenyewe.
 
Postinor-2 (P2): Ukweli nikwamba matumizi ya mara kwa mara ya p2 yanaweza kuwa na athari kubwa kwa mtumiaji, Mbaya zaidi imeripotiwa kuwa ni chanzo kikubwa cha ugumba kwa wanawake
 
Nje na hapo matumizi ya kiholela ya madawa haya hupelekea magonjwa hatari ikiwemo saratani ya shingo ya kizazi
 
Kwa asilimia kubwa vidonge hivyo hupelekea mabadiliko ya mzunguko wa hedhi, Kuona hedhi mara 2 kwa mwezi au kutoona kabisa, Pamoja na tatizo la Uke mkavu, na maumivu wakati wa tendo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…