Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matumizi ya dawa hizi bila ushauri wa daktari nihatari kwani inaweza pelekea matatizo ya moyo na hata kifo cha ghafla
 
ASPIRIN: aspirin ni dawa muhimu sana lakini inaweza kuwa hatari ikitumiwa kiholela kwa sababu sio salama kwa kila mtu.
 
Dawa hii inajulika kwa ubora wake wa hali ya juu ya kutuliza maumivu na wakati mwingine hutumiwa kutuliza homa
 
Inaweza kusababisha chakula kisisagike vizuri hali ambayo inaweza kumsababishia mtu kupatwa na vidonda vya tumbo.
 
Inaweza kuwafanya watoto kupata na ugonjwa hatari unaojulikana kama (Reye syndrome) ambayo inaweza kuathiri (ini au ubongo).
 
DICLOFENAC: Matumizi ya kiholela ya dawa za kupunguza maumivu na uvimbe huchangia ongezeko la hatari ya kupata maradhi ya moyo.
 
Dawa kama vile Ibruprofen, Naproxen na Diclofenac ndizo dawa hutumiwa sana kupunguza maumivu na uvimbe.
 
DICLOPAR: Sikuhizi watu wakimeza Paracetamol wanadai kwamba haitulizi maumivu na kukimbilia diclopar.
 
Nidawa hatari sana kwa afya yako, endapo utaitumia bila ushauri wa daktari, Ukitumia dawa hihi mara kwa mara inaweza pelekea Matatizo ya mifupa na joints hapo badae.
 
FLAGYL (METRONIDAZOLE),, Dawa nyingine ambayo inatumiwa vibaya inafahamika kama flagyl.
 
Baadhi ya watu huzinunua bila maelekezo ya dakatari. Wapo wanawake wameigeuza hii dawa P² au za kutolea mimba Nihatari sana kwa afya kutumia dawa kwa kutegemeana faida kwenye side effects...Hapo nikujimaliza mwenyewe.
 
Postinor-2 (P2): Ukweli nikwamba matumizi ya mara kwa mara ya p2 yanaweza kuwa na athari kubwa kwa mtumiaji, Mbaya zaidi imeripotiwa kuwa ni chanzo kikubwa cha ugumba kwa wanawake
 
Nje na hapo matumizi ya kiholela ya madawa haya hupelekea magonjwa hatari ikiwemo saratani ya shingo ya kizazi
 
Kwa asilimia kubwa vidonge hivyo hupelekea mabadiliko ya mzunguko wa hedhi, Kuona hedhi mara 2 kwa mwezi au kutoona kabisa, Pamoja na tatizo la Uke mkavu, na maumivu wakati wa tendo
 
NB: Hutakiwi kutumia njia hii zaidi ya mara moja kwa mwaka madhara yake Unaharibu balance ya homoni kwa kiwango kikubwa kwa mtumiaji sugu hupelekea Ugumba
 
MITISHAMBA : Sikuhizi imekuwa kimbilio la wengi sana huku wakisahau madhara makubwa yanayo tokana na matumizi ya madawa hayo ya mimba...
 
Dawa nyingi hazijafanyiwa utafiti wa kina, hivyo zinaweza kusababisha athari zisizotarajiwa.
 
Baadhi ya watu hupata mzio au athari za kiafya kama vipele au matatizo ya kupumua. Allergies (Mzio)
 
Mitishamba inaweza kupunguza au kuongeza athari za dawa za kisasa, hivyo kusababisha matatizo makubwa ikiwa ni pamoja na Usugu wa vimelea dhidi ya dawa. Tunaona watu wanao ishi na UTI since darasa la 7 mpaka mama wa miaka 37.
 
Back
Top Bottom