myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Kweli kabisa hiliMaisha ya shule, yalitufunza sio kila aliyesema hajasoma basi hafaulu mtihani hapana, kuna muda unahitaji bahati zaidi kuliko juhudi zako
ππMaisha ya shule, hayatukupa marafiki wa dhati sana sababu ya kuzoeana sana na kuchukuliana poa, lakini yametupa watu tunaofahamiana nao kila idara.
πππMaisha ya shule, hapo yalitufunza hakuna usawa katika maisha, tulivaa sare moja lakini kila mmoja alitokea katika familia zenye hadhi tofauti kiuchumi, baada ya masomo wapo walioandaliwa na sisi tuliojitafutia.
β οΈβ οΈβ οΈMaisha ya online sio maisha halisi, mtu anaweza kupost Kala kisinia kumbe usiku Kalala njaa, post yake niya miaka mitatu iliyopo pita".
Hapa ndio penyeweUsiombe maisha ya haraka, omba moyo wa uvumilivu. Maana baraka halisi huwa haziji kwa ghafla, hujengwa taratibu. Kama wewe ni mvumilivu, basi tayari una nusu ya mafanikio.
Hapo sasaKuna mtu anafanya mambo ya hovyo, na maisha yake yanaenda fresh.Na kuna mtu anafanya mambo yake kwa usahihi kabisa, na maisha yanamuendea hovyo..Maisha hayawezi kutenda haki kila wakati.
Watu wanataka ufanye kile waachoona wao ni sawa,usipofanya unaonekana mshamba na kutukanwa kabisa.Dunia ina mengi,hatuwezi wote kufanya mambo yanayofanana na ikiwa hivyo maisha yatakua yanaboa,utofauti ndio ladha ya maisha yenyewe.Ishi maisha yako halisi.
Wapumzike kwa amani π π€²
AminMungu atupe siku njema yenye amani na utulivu π€²
AminMungu awaponye wagonjwa wote π π€²
ππSiku njema wadau wa daladala bodaboda bajaji na kwenye vivuko
ππMlio safarini mfike salama muendako
ππSiku njema mlio maofisini leo
Siku njema wakulima wafugaji wavuvi na wamachinga wote
ππSiku njema Wauguzi na Madaktari wote