Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_20250706-021907_Web Browser.png
 
Siku ya leo, Rais Samia kazindua rasmi hema (jengo?) la kanisa la Rise and shine (Kanisa la Mwamposa) kwenye viwanja vilivyokuwepo kiwanda cha Tanganyika Packers. Imeelezwa jengo (hema) hilo lina gharama ya zaidi ya bilioni 15.

Huenda ndio gharama za juu zaidi kuwahi kutokea hapa Tanzania kwa taasisi za kidini kumiliki. Hakuna kanisa wala msikiti uliowahi kuelezwa kujengwa kwa gharama kukaribia bilioni 15 hapa Tanzania. Na bila kumumunya maneno, ujenzi wa gharama hizo unaashiria kilichotengenezwa pale ni kitu chenye miundo mbinu ya kudumu katika eneo lile.

Lakini uzinduzi huo umezaa utitiri wa maswali, na vyema tukayajadili hapa ili kuweka wazi sasa ili huko baadaye isije ikaleta maneno, mivutano na kushikana masharti.

1. Je, serikali imeamua kummilikisha rasmi Mwamposa lile eneo?

2. Je, serikali imebadili matumizi ya eneo lile kutoka kuwa kiwanda kilichokufa au eneo la wazi la kutumiwa kwa matukio ya kupita na kuwa eneo rasmi binafsi la taasisi ya kidini?

3. Je, serikali imefuta uwezekano wa mtu au taasisi zingine tofauti na Mwamposa kutumia eneo lile kwa sasa au baadaye?

4. Kisheria lile eneo lilikuwa likimiliwa na nani, na matumizi ya sasa (kidini) yanamfaidisha vipi mmiliki?

5. Kwa hatua hizi za sasa, je inaashiria serikali haina tena mpango, mikakati au mawazi kuja kufufua kiwanda cha Tanganyika Packers?
 
Back
Top Bottom