myoyambendi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2013
- 174,811
- 721,144
Kimsingi twapaswa kujua katika maisha, wale watu ambao hukutegemea kabisa kwamba siku moja watakuja kukusaidia ndiyo huwa wa msaada kwako, na wale ambao wewe ulikuwa na matumaini nao wanakuja kukuangusha na wasambaza chuki dhidi yako, tenda wema nenda zako usingoje shukrani
Wanavyokudhania na kukuchukulia sivyo ulivyo, ukarimu wako na unyeyekevu wako kwao ndiyo unaokuponza. Ila Usibadilike kwa sababu yao. Endelea kuwa Mtu mwema.
SawaSilaha pekee ya mafanikio ni kuthubutu na kujiamini , kwa kila jambo unalolifanya na kuamini kwamba utafanikiwa . Kutokujiamini na kukata tamaa ndio anguko letu Vijana wengi wa kitanzania
Silaha pekee ya mafanikio ni kuthubutu na kujiamini , kwa kila jambo unalolifanya na kuamini kwamba utafanikiwa . Kutokujiamini na kukata tamaa ndio anguko letu Vijana wengi wa kitanzania
Sawa piaKukumbuka ulikotoka ni faraja katika maisha, kuwakumbuka waliokusaidia na kukufikisha ulipo Leo ni hatua katika maisha, kujisahaulisha na kuwafitinisha na kujifanya huwatambui waliokusaidia ni ukosefu wa hekima
👍👍👍Kukumbuka ulikotoka ni faraja katika maisha, kuwakumbuka waliokusaidia na kukufikisha ulipo Leo ni hatua katika maisha, kujisahaulisha na kuwafitinisha na kujifanya huwatambui waliokusaidia ni ukosefu wa hekima
Ukiona watu wanakufuatilia sana usikasirike, jua Wewe ni kioo kwao unawaonyesha njia. Wengi wao wanashindwa kukuambia kwasababu ya kiburi chao, wewe endelea kuwapenda na kuwajali, usiwachukie
Ukiona watu wanakufuatilia sana usikasirike, jua Wewe ni kioo kwao unawaonyesha njia. Wengi wao wanashindwa kukuambia kwasababu ya kiburi chao, wewe endelea kuwapenda na kuwajali, usiwachukie
Wanavyokudhania na kukuchukulia sivyo ulivyo, ukarimu wako na unyeyekevu wako kwao ndiyo unaokuponza. Ila Usibadilike kwa sababu yao. Endelea kuwa Mtu mwema.
Kuumia ni sehemu ya maisha, kakuumiza, kakupotezea muda, kakukimbizia wenye maana katika maisha yako, na pia anaendelea kukufuatilia, msamehe nenda zako watakuja wenye maana zaidi yake , maisha ni hatua , piga hatua nyingine , lakini usirudi nyuma, ipo siku atakukumbuka .