Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye haya maisha meza inaweza kugeuka muda wowote. Ukiwa juu jifunze kuwa mnyenyekevu na ukiwa chini kuwa na matumaini.
 
Siku ukiwa mgonjwa ndio utajua kuwa afya ndio kitu muhimu kuliko vyote maishani.
 
Tunatofautiana sana wakati wengine wapo mjini kutafuta kazi wengine wamekuja kutafuta pesa
 
Ili ufaulu mtihani lazima usome. Ukitaka kufanikiwa kwenye maisha lazima uweke akiba. Tengeneza kesho yako leo.
 
Ili ufaulu mtihani lazima usome. Ukitaka kufanikiwa kwenye maisha lazima uweke akiba. Tengeneza kesho yako leo.
 
Usilazimishe kukupata kile unachokitamani lazimisha kupata kile unachokitaka
 
Ishi maisha yako usiige jiangalie wewe songa mbele kila mtu alishapangiwa maisha yake na mungu
 
Lengo kuu la wewe kuja duniani ni ili uyaendeshe maisha sio maisha yakuendeshe wewe. Kila kitu kipo ndani ya uwezo na unaweza kukipata ukijitambua na kuamua.
 
Lengo kuu la wewe kuja duniani ni ili uyaendeshe maisha sio maisha yakuendeshe wewe. Kila kitu kipo ndani ya uwezo na unaweza kukipata ukijitambua na kuamua.
 
Rafiki wa kweli hawezi kuogopa kukuambia ukweli ukikosea. Na hawezi kukusifia ukifanya ujinga
 
Nidhamu ni pamoja na kujiheshimu mwenyewe kama hujiheshimu hutaheshimiwa na kama huna nidhamu maana yake watu watakuzoea na baadae kukufanyia wanavyotaka. Kuwa na nidhamu na weka mipaka kwenye maisha yako binafsi.
 
Kama mambo hayajaenda vile ulitaka usipanic, kujiona huna bahati au una mikosi. Tuliza akili fikiria wapi wewe mwenyewe ulikosea. Tafuta njia tofauti ya kulifanya tena. Halafu pia angalia fursa nyingine inawezakana hiyo sio fani yako. Usijilaumu kwa kujaribu.
 
Sometimes kwenye kufurahia maisha huitaji mtu mkamilifu saaana. Mtu awe tu na mood, dress well na awe tayari kucelebrate the day, asiwe na wenge inatosha sana
 
Kwenye mahusiano kila mtu anafanya kitu huku akijua anachokifanya. Hamna cha bahati mbaya au kukosea. Na hata huo msamaha anaomba kwa vile umegundua tu sio kuwa anajuta kivile.
 
Kwenye mahusiano kila mtu anafanya kitu huku akjjua anachokifanya. Hamna cha bahati mbaya au kukosea. Na hata huo msamaha anaomba kwa vile umegundua tu sio kuwa anajuta kivile.
 
Kama ukiweza kufanya vizuri kwenye jambo linalokuhusu na kukupa faida inatosha. Mengine acha wengine wafanye.
 
Bora kuheshimiwa kuliko kupendwa. Watu wakikupenda watajiweka karibu halafu watakuzoea. Wakishakuzoea heshima itapungua. Lakini wakikuheshimu hawawezi kukuzoea na hawatajua undani wa maisha yako.

Chagua kuheshimiwa
 
Mtu umeshaamua kwenda mbele sasa unaangalia nini nyuma. Angalia unapokwenda ya nyuma yaache yabaki na uliowaacha huko hayakuhusu tena.
 
Usiweke mambo yako wazi kwa kila mtu. Hata marafiki unaowaamini nao wana marafiki zao ambao inawezekana hawakupendi.
 
Kijana mwenzangu usidharau mafanikio yako hata kama ni kidogo kiasi gani. Kesho yako kubwa na ya ndoto zako inaanza kujengwa na kidogo ulichonacho sasa. Tena usiruhusu watu wadharau ulichonacho, kwani hawakuwepo wakati unatokwa jasho kukitafuta. Pambana amini kesho yako ni kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…