Kwenye chumba chenye giza ukiwa unaangalia movie yenye mwanga utaona mwanga, kwenye chenye mwanga ukiangalia movie yenye giza utakuwa unaona giza, kuona ni zao la kile ulicho focus, haijalishi mazingira yako yana nini bali wewe macho yako yana tizama nini
Usiruhusu mtu yeyote akuondolee heshima yako. Kumbuka, jina lako ni urithi wako mkubwa kuliko pesa, na tabia yako ndiyo urithi utakaoachia watoto wako.
dunia ya sasa imejaa watu wanaosema wanakupenda lakini matendo yao ni kinyume. Usijaribu kuharibu heshima yako kwa kujaribu kupendeza kila mtu. Mapenzi ya kweli hayaji kwa maneno pekee – huja kwa vitendo, heshima na nidhamu.
Usisahau, kuna watu watajaribu kudhihaki ndoto zako. Watajaribu kukunyima matumaini. Lakini mwanangu, kumbuka… mti unaokua chini ya dhoruba una mizizi thabiti zaidi. Vile vile, unaposhindwa, usipoteze roho yako… kila kushuka ni nafasi ya kupanda tena kwa nguvu zaidi.
Upendo wa kweli haujengwa kwa mzaha na maneno pekee. Una nguvu, heshima, nidhamu na ukweli. Ukijua hii, maisha yako ya mapenzi yatajenga, hayataharibu moyo wako. Usikubali kuishi kwenye uongo wa hisia tu; chagua hekima, heshima na moyo thabiti.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.