wanyama hawa
huogopwa hata na wanyama wenzao wanao
winda kwani bifu lao huwa ni lakufunga mtaa,
hata simba akiwaona mkia wake huuficha,
usiseme kwa fisi nk,
TWIGA ni miongoni mwa wanyama wenye
mvuto mkubwa kutokana na uzuri na mambo
kadhaa ambayo yanatokana asili yake ikiwa ni
zawadi kutoka kwa Mungu… ndio maana hapa
nchini Tanzania tunamtumia kama alama ya
urithi wa Taifa.
Twiga ni mnyama aliyeambatana na sifa nyingi
ukilinganinisha na wanyama wanaopatikana
hapa duniani, kwani ni mrefu kuliko wote
duniani, ana miguu mirefu,shingo ndefu sana,
ulimi mrefu.
Huku sifa nyingine za ziada kutoka kwa
mnyama huyu anayeaminika kuwa na maringo
kuliko wote ni kuwa na pembe fupi zilizo butu,
wakati huo huo mwili wake ukiwa na mabaka
yenye rangi ya kahawia-njano na kuzungukwa
na rangi ya maziwa.
Mnyama huyu anapatikana katika nyika
hususan sehemu zenye migunga, ‘Vkwata’
pamoja na mikakaya,miti ambayo huifurahia
sana kwani ndio ni chakula chake kikuu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.