Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kifupi: Malkia Isis alikuwa mungu wa muhimu katika Misri ya kale. Alizaliwa na Nut (mungu wa anga) na Geb (mungu wa dunia). Alikuwa na kaka wawili: Osiris, Seth na dada mmoja: Nephthys. Ndugu wote hawa walikuwa pia ni miungu. Baadaye aliolewa na kaka yake Osiris na wakazaa mtoto wa kiume aliyeitwa Horus. Baadaye kulizuka bifu la kugombea madaraka na Seth akamuua Osiris na ili kukata mzizi wa fitina kabisa akamkata kata vipande vipande na kuvitawanya sehemu mbalimbali za Misri; na kujichukulia madaraka. Hata hivyo ISIS alifanikiwa kuvikusanya vipande vya kakake (na mumewe) Osiris na akaweza kumfufua kwa kutumia nguvu zake za Magic.

Isis anaonekana kama kiwakilishi cha mama mkamilifu kutokana malezi sahihi aliyompa mwanawe Horus. Inasemekana hata taswira za Bikra Maria kama mama mkamilifu kwa mwanawe Yesu Kristo zimetokana na malkia huyu wa kale kutoka Misri. Anatazamwa pia kama mke bora aliyekuwa tayari kumpigania mumewe hadi kumfufua. Alikuwa mungu wa muhimu aliyeabudiwa ndani na nje ya Misri na mpaka leo anaabudiwa na watu mbalimbali duniani.

Sis. I am done. Kama nimekosea mahali unaweza kusahihisha.
a9fbab997e522b1cc9ff834d617520db.jpg
9e9de8365f0c1672d5163f9c3b093ddc.jpg
God job shimba hakika ujakosea sehemu yoyote 100% sahihi
 
Back
Top Bottom