Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Serikali ya Nigeria imeagiza police kumkamata Peter Okoye "P-Square" baada ya kuwakoromea na kuwafumua viongozi wa serikali Kwa kuwaita "mad and stupid" baada ya serikali kutoa azimio la kupiga marufuku wasanii wote wa Filamu na muziki kushuti kazi zao nje ya Nigeria Uamuzi ambao umepingwa vikali na asilimia 99% ya wasanii wa nchi hiyo kwa kusema iweje wao wapiganie tasnia hizo kwa shida kubwa kwa miaka mingi bila support ya serikali na Sasa serikali hiyo hiyo inakuja kibabe kupitisha Sheria zisizo rafiki bila hata kuwashirikisha wasanii wenyewe Sehemu ya andiko la serikali ya Nigeria ikionyesha ubabe flani inasema..... "We urge the security agencies in the country to arrest Mr Peter Okoye for disrespecting our government and bringing it to a disrepute. If you cannot produce in Nigeria and hire Nigerians, then leave the industry. We must export Nigerian culture to the outside world through our music and videos" . . . TOA MAONI YAKO HAPA
 
Msanii Linah Sanga 'Ndege Mnana' amekanusha taarifa zinazoenea mtandaoni kuhusu suala la kujifungua na kuwataka watu wazipuuzie huku akiwasihi mashabiki zake waendeee kusubiri taarifa iliyo sahihi kutoka kwake na kwenye mitandao yake ya kijamii. Linah amekanusha taarifa hizo kupitia EATV na kusema kwamba anashangazwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni huku akiwa hajui mtu anayesambaza taarifa hizo ana malengo gani. "Hongera ya nini mbona mimi bado mjamzito? Sijajifungua bado na hata mwenyewe nashangazwa na huyo mtu aliyeanza kusambaza taarifa hizo ana malengo gani? Nawaomba mashabiki zangu waniombee kwa sasa hivi nikiwa nakaribia kwenda kujifungua hivi karibuni ingawa siwezi kusema ni lini kwani siyo vizuri, watu wanatakiwa waone. Mungu akinisaidia taarifa watazipata kupitia kwangu mwenyewe au kwenye mitandao yangu ya kijamii," Linah alifunguka . Katika hatua nyingine Linna ameongeza kwamba sababu ya za kutoonekana sana kipindi cha hivi karibuni hakujasababishwa na kisirani, hivyo kutoonekana kwake zipo sababu ya msingi. "Ukweli nina sababu zangu za msingi zinazonifanya nisionekane, Ninachomshukuru Mungu kuwa na mimba hakujanifanya niwe kisirani ila baada ya ya sababu zangu kuisha nitaonekana kama kawaida. Niombeeni nijifungue salama", aliongeza Udakutz inamuombea mwanamuziki Linah maandalizi mema ya kumpokea mtoto wake wa kwan
 
SERIKALI imetoa onyo kwa watumishi wa umma wanaotoa siri za serikali na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa watachukuliwa hatua za kisheria. Onyo hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki (pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa watumishi wa umma wa Manispaa ya Ubungo. Kairuki alisema mtumishi wa umma atayejihusisha na usambazaji wa taarifa za serikali, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani na kupewa kifungo cha miaka 20 jela. Alisema serikali ina utaratibu wake wa kutoa taarifa kwa umma ikiwa ni pamoja na kupitia machapisho yake kwa jamii. .
 


Umenena

Waliopitwa waisome tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…