Uzi maalum wa kuwakumbuka Walimu waliotufundisha kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu

Uzi maalum wa kuwakumbuka Walimu waliotufundisha kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Tukiachana na Mpwayungu Village ambaye usiku na mchana yeye ni kuwasakama walimu, tupo sisi wengine tunaoheshimu na kuthamini mchango wao kwenye maisha yetu ya kila siku.

Walimu wangu wa chekechekea kuna Teacher Mary, Umoja Primary School.
Mama Stambuli, mama mzazi wa Azza, amenifundisha pia prep Umoja.

Mama yake Shikunzi, Anna Mgaya, amenifundisha Primary Umoja. Mr. Lohah alikuwa mwalimu wetu mkuu.

Sisimba nimefundishwa na Richard Kasela mtu mwenye vipaji vyake lukuki, Mwaisaka mkali wa hisabati.

Mtawa na Msuya ndio walikuwa walimu wakuu. Muchuruza, Nyandindi, Mapunda, Mwaisumo, mwl Matthew (mama yake William Mpangala), mwl Benard (mama yake Edmund Ntalugela), mwl Chang'a na wengine heshima kwenu.

Walimu wangu wa sekondari hasa Yisambi Reka Ntipoo, gwiji la hisabati you are the best teacher ever. Mwl Mageta mwalimu wangubwa Commerce na Book Keeping ulinijengea msingi imara wa mimi kuwa hivi nilivyo leo, Mwalimu Mwangoka alikuwa mwalimu mkuu pale Meta. Miss Jackson (Mrs Alinani Mwakalindile a.k.a Mama Niti) ulinifanya niijue vizuri Geography na nitamaniniizunguke dunia. Namshukuru Mungu nimeenda Australia, America Kaskazini (Canada 🍁 na USA 🇺🇸) sijaenda Mexico tu, nimezurura America Kusini, Asia, Ulaya, na Africa nyumbani.

Chuo pale Doriye ndio alikuwa principal wetu. Cleopa, madame Irene, Ndasa na wengine wengi nawashukuru sana. Shukrani na heshima kwenu.

Mungu awabariki sana walimu wote wa Tanzania
 
Asante mwalimu wangu mama yangu kipenzi, amekuwa mwalimu wangu nyumbani mda wote na amenifundisha vitu vingi na mafanikio yangu yanatokana na mafundisho yake.

Asante Mama kwa Elimu yako bora.
Mzazi ni mwalimu namba moja anayefundisha bila malipo ya mshahara
 
Back
Top Bottom