Uzi maalum wa kuziombea timu za Tanzania Simba na Yanga, zote zifuzu hatua ya makundi CAF

Uzi maalum wa kuziombea timu za Tanzania Simba na Yanga, zote zifuzu hatua ya makundi CAF

Mimi Simba ila utopolo walishawai kutufanyia unaa mkubwa sana kuwapa ushirikiano wa hali na mali wageni wanaocheza na Simba.

kuwaambia wapinzani wa Simba,"wasile chakula,maji wala juisi,wasiwashe ac hapo hotelini,vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji wadeki na maji ya moto",,huu sio uungwana kabisa ni kuipaka matope Simba ionekane wameweka Sumu.
Hapo walifanya ujinga kwa kweli
 
Hivi kwanin Tanzania Kisoka hatuna ushirikiano?

Tutambue kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Umoja wetu watanzania ndio uliotuwezesha kumshinda Idd Amin Dada mwaka 1978/1979.

Nawaomba wapenzi wa soka la Tanzania wote tuungane katika maombi na kupeana mbinu mbali mbali ili Tim zote zifuzu hatua ya makundi.

Tuache ushabiki hautatusaidia, hii ni Vita Kama Vita vingne, tutangulize utaifa Kwanza.

Wachungaji,Mapadre hata Mashehe karibuni mtoe maombi yenu.

Pia hata wataalam toeni ushaur kwa tim zote mbili kwamba inatakiwa zifanye nin ili zishnde mech za leo.
Timu zote mbili zikiingia makundi,Tanzania itaheshmika mno kimichezo.

NB: Utopolo tumsamehe kwa makosa ambayo anayafanyaga ya kuwapokea maadui na kuwafundisha mbinu pale wanapokuwa wanakuja Tanzania kucheza na Simba.

Karibuni kwa dua, Sala na ushauri pia
Hivi mbona sisi wa Azam na Kipanga mnatupitipa kama hamtuoni vile. Sawa dua la kuku

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom