Uzi maalum wa maisha, halisi huko mtaani kwenu kwa sasa.

Abbasfarudume

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2017
Posts
1,625
Reaction score
1,326
Sie huku mtaani kwetu, vyuma vimekazwa! Mpaka mbuzi wanakula chips, na Mbwa wanakula mahindi ya kuchoma, na miwa. Sijui Uswaz kwenu kukoje huko wakuu....!
 
Hapa kwetu mbuzi wameanza kula maharage na kunywa mchuzi wa nyama. Nadhani kwa miaka kadhaa ijayo tutaanza kushuhudia wanyama wanaumwa magonjwa ya binadamu. Unaenda nyumbani kwa MTU unaambiwa "usimshtue huyo kuku, ana presha" au "yaani mimi sijui nifanyaje, nguruwe wangu wote wanaumwa kisukari. Sijui ma miwa haya wanayokula!!!?"

IRONS ARE KAZED
 
[emoji23] [emoji23]
 
Duuh! Hatari sana mkuu hiyo!
 
Huku kwetu njia za zamani zimeota nyasi vichochoro vimeongezeka watu wanakwepa madeni. Ndoa zipo kwenye hali tete sana, majini, dagaa ndio mboga nyama imekuwa anasa. Idada ya wanywa gogo ndio usiseme
Tutafika kweli mkuu?
 
Ulikua unamtishia nani kuondoka JF?
 
Reactions: BAK
Hii safari ni ngumu ila tutafika kwa mbinde mkuu. Yaan sasa hivi kukutana na mtu kapishanisha vifungo vya shati au kavaa viatu rangi tufauti mchukulie poa tu maana wote si vichaa bali ni vyuma vimekaza tena vya mjerumani mkuu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Sio ya kucheka, vitu vingine vinachekesha mkuu!
 
Hahahahaa aisee Cheka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…