Uzi Maalum wa maswali na masuala mbalimbali yahusuyo Kodi, ushuru na masuala mengine yanayowahusu TRA

Hili silifahamu kwa kweli,ngoja na mimi nisubirie majibu ya wanaojua...
 
Hapo cha kufanya ni kuandika barua kwa meneja wa tra/mkoa au wilaya sehemu ulipofungulia hilo file, ziwe mbili hata ukimpata mtu anayekwenda mwanza unampatiaa anazipeleka zitagongwa mhuri moja itabakia huko nyingine watampatia, unakuwa umemaliza baada kama ya wiki moja file litahamishiwasehemu uliyoitaka. Lakini kwa simu utakesha.
 
Ni kwamba ulikua na biashara huo mkpa ukahamisha ama ulikata tin kwa matumizi ya leseni etc?
 
Nshafanya hiyo, pigia mtu simu alieko mkoa unaohama aende pale TRA mkoa utokao akaongee nao physically. Wakati huo TRA wa huku wanatuma mail yenye scanned letter uliyoandika kwa meneja wa kule. Anachoenda kufanya huyo jamaa ni kupush hao wa mkoani wahamishe details zako kuja mkoa unaotaka.
 
2. Malipo
Nakushauri nenda tawi jingine na waombe moja kwa moja statement ya malipo ya kodi unayotaka kulipa, utasaidiwa. Leta mrejesho km utaenda Tax Service Centre nyingine
 
Yani umeshindwa kuwaambia wakusaidie kukupa muongozo unakuja kutusumbua huku. Aya Njoo nikueelekeze ila utafidia muda wangu
 

Hao TRA ndo wenye hilo jukumu la kuhamisha. Ulipaswa hayo maswali uwaulize ulipokuwa nao ofinini. Sasa unatuuliza huku ili tukakusaidiekuuuliza au?
Humu pia kuna watu wa TRA yawezekana wakakusaidia
 
Wadau nimeleta mrejesho..Ukifika TRA kuna barua ya maombi ya kihamisha TIN ambayo unaijaza, inasainiwa na Manager kisha inatumwa kwa Manager wa tawi ulikotoka ili TIN yako ihamishwe....ni swala la muda mfupi tu TIN inakuwa imehamishwa na unaweza kufanya malipo...Asante sana wadau kwa ushauri wenu na maoni yenu.
 
Asalaam Alyekum,
Tumsifu Yesu Kristo wanajamvi,

Leo nimeona bora nawajulishe wanajamvi pia TRA kupitia hizi kurasa zetu pendwa za JamiiForums ya kwamba kituo cha mafuta cha Lake oil kilichopo Buguruni Malapa jiji Dar-es-Salaam hawatoi risiti pindi unapoenda kununua mafuta, kisingizio chao kikubwa ni kuwa machine zimeharibika.

Sasa taarifa kwenu TRA, wamulikeni hawa Lake Oil maana miezi miwili nyuma nililiona hili nikaona sio kesi ila wiki jana nikapewa tena taarifa hiyo hiyo kuwa machine za risiti ni mbovu.

TRA, ni kweli mnakaa miezi miwili bila kwenda kutengeneza zile machine za risiti?

Usiku mwema wapendwa.
 
Kuna sehemu nyingi sana huwa hawatoi risiti ila ww umeona ni hicho kituo tu. na hiyo inaonyesha ni kiasi gani unachuki na hicho kituo cha mafuta.
 
Mkuu, bilashaka ulienda na gari na ndio ukakutana na dhahma hiyo.
Basi naomba nimupongeze tu kwamiliki chuma huko Daslam, hayo ya riaiti minaona ni umbeya tu chunga usije ukasutwa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…