Uzi Maalum wa Visa vya Nyumba za kupanga

Uzi Maalum wa Visa vya Nyumba za kupanga

wingatereza

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2016
Posts
1,334
Reaction score
1,722
Wadau Umuofia kwenu.

Nilikutana na visa kadha wa kadha katika maisha ya nyumba za kupanga. Kimojawapo ni wenye nyumba kuamuru wapangaji tujisaidie choo cha peke yetu na wao cha kwao, lakini cha ajabu choo chetu kila asubuhi tunakuta mtu kanya pembeni.

Tukalalamika weeee siku nikaamua kwamba sitatumia choo hicho badala yake nitatumia cha wenye nyumba. Nikafanya hivyo.

Matokeo: Niliugua ugonjwa usiojulikana mpaka baada ya kuteseka na kutumia gharama nyingi hospitali, jirani mmoja akanitobolea siri nihame. Siku mbili baada ya kuhama nikapona full yaani 💯💯

Share experience yako ya visa ulivyokutana navyo hata vya kimapenzi.
 
Tuliwahi ishi Iringa miaka fulani maeneo ya Kihesa mke wangu akapishana lugha na Dada wa kaka mwenye Nyumba weeee ... ilibidi tuhame 😂😂😂
 
Ilikua kila wife aikanza kupika nyama asipo wapa wapangaji wenzie wana kasirika halafu kila Umeme ukiisha nikitoa mapema wanasema najifanya nninahela
 
Ilikua kila wife aikanza kupika nyama asipo wapa wapangaji wenzie wana kasirika halafu kila Umeme ukiisha nikitoa mapema wanasema najifanya nninahela
Ndo kinachonitokea saa hizi siku hizi tunaambia hatunaa...!! Wapuuzi sanaa yani wambea mbea tu
 
Kupandishiwa pesa ya umeme kila week kisa ameniona na laptop [emoji23]
 
Back
Top Bottom